Home » » Papaa Ze Blogger Kucheza Filamu Ya Siku Za Mwisho ---666 (End Time)

Papaa Ze Blogger Kucheza Filamu Ya Siku Za Mwisho ---666 (End Time)

 papaa ze bloger akiwa katika pozi



FILAMU YA SIKU ZA MWISHO ZAENDELEA KUCHEZWA IS COMING SOON


Soko la "Christian Movies" ambalo kwa Muda Mrefu limekuwa likishikiliwa na Watu walio nje ya "Ufalme wa Kristo" linaingia katika ushindani baada ya Wakristo Mbalimbali Kuamua Kuingia katika Soko hilo ili kuweza kufikisha Ujumbe wa Neno la Mungu Halisi usio Chakachuliwa na Pia Kufikisha Ujumbe Sawia.

Emmanuel Myamba almaarufu kama Pastor Myamba amekuwa akicheza vizuri zaidi Christian Movies sababu yeye pia ni mtu ambaye yupo kwenye upande unaofahamu nini maana ya nguvu za Mungu na vile zinavyotenda kazi. Katika Filamu yake iliyokamilika na kuingia kwenye soko muda mrefu nguvu za Mungu zilionekana live pale mapepo yalipolipuka Kikwelii wakati wa Shooting.

Filamu Mpya inayotengenezwa inayokwenda kwa jina la "Siku Za Mwisho" a.k.a "End Time" ipo katika hatua za Kukamilika na Mapema Mwa Mwanzoni mwa Mwezi wa August Filamu hiyo itaachiliwa katika Soko la Tanzania na Nje Ya Tanzania.

Filamu hiyo yenye Kusudi na madhumuni ya Kuwakumbusha Wakristo Safari Ya Mbinguni, lakini Pia Kuhusu Unyakuo na Watu Watakavyoishi mara baada ya Unyakuo Wa Kanisa hapa Duniani. Filamu hiyo iliyoandaliwa na Mch. Joshua Kaduma na kuwa Directed na Mr. Mtitu imekuwa ya aina yake sababu filamu hiyo imekuwa ikigusa hata washiriki pamoja na Wanao shoot na kusema hakika kazi hii haitakuwa Bure.

Weekend hii Blog ilizungumza na Mch. Joshua Kaduma na kutaka Kujua maendeleo ya Ukamilishaji wa Filamu hiyo, Mchungaji alikuwa na haya ya kusema "Filamu hii ilianza kama ni Somo la Siku Za Mwisho nililokuwa nikiandaa KWa ajili ya Kanisa ninalochunga, Wakati nilipokuwa nikiandika Somo, Roho Mtakatifu akaanza Kunipa picha, ya maisha halisi ya Kwetu Tanzania yatakavyokuwa Wakati wa Unyakuo, Niliingia kwenye Maombi Mazito na Kumwomba Mungu aliasaidie Kanisa lake. Nilipomaliza Somo, Mungu akanisemesha kwa habari ya kutengeneza Filamu, Nikachukua Notes za Somo nikaenda nazo kwa Wataalamu wa Script Waliposoma somo, na ile Mifano, Wakasema ni Script tosha inayoweza kutengeneza Movie ya Tofauti hapa Tanzania, ndipo Idea ya Movie ikaja rasmi".

Akiendelea kuongea na Mchungaji Kaduma alisema "Mpaka Sasa Filamu Imekamilika kwa sehemu kubwa zimebaki Sehemu Chache za Shooting, na editing na mwisho kabisa mwanzoni mwa mwezi wa nane itakuwa Sokoni. Sasa tunataka Kanisa Kuhubiri kwa njia nyingine kufikisha injili ya Yesu Kristo katika Kizazi hiki".
Msanii wa filamu dokii ambaye pia amecheza katika filamu hiyo


Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog