Pastor Myamba Na Dhana Nzima Ya Uhalisia Katika Uigizaji
Mr Emmanuel Myamba ni
mtumishi wa Mungu,ameokoka na anasali katika kanisa la Living Water
Kawe Makuti lililo chini ya Mtume Onesmo Ndegi.Tofauti na utumishi
Myamba ni muigizaji wa Filamu maarufu nchini Tanzania.katika moja ya
washa aliwahi sema kuwa “Ni wazi ukiangalia filamu zetu zinakosa weledi
katika uandishi wa miswada, uongozaji, uhariri na hata uumbaji wa
wahusika. Lazima tukubali udhaifu huu turekebishe” aliendelea kueleza
kuwa “Nimekuwa katika tasnia ya filamu kwa muda sasa lakini kuna
changamoto nyingi katika tasnia ya filamu, na jambo ambalo nimeliona ni
wasanii kukosa ujuzi kitaaluma katika utendaji wa filamu kwa ujumla, kwa
mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii maskini
wasio na uwezo wa kulipa ada kubwa katika vyuo vilivyopo, lakini pia
kutoa nafasi kwa wale ambao wanafanya kazi lakini taaluma imekuwa shida
kwao, na mwito ni mkubwa kweli,”
“Tatizo
kubwa la wasanii wa Tanzania kushindwa kufaidika na vipaji na ujuzi
wao, ni kukosa elimu ya kutosha ya mambo ya sanaa, kwa mantiki hiyo
nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii, nimeapa kwamba
nitaweka ada ndogo ili wasanii wachanga au kwa ujumla tuseme wasio na
uwezo mkubwa wa kifedha waweze kusoma hapa,”
Kati ya waigizaji wanaoigiza kwa hisia na kuvutia nyoyo za mashabiki hapa Tanzania basi hutakosa kumtaja Emmanuel Myamba a.k.a Pastor Myamba ambaye mara nyingi tumezoea kumuona akiigiza kama mchungaji au mtu mwenye maadili ya dini.
Mimi
kama mdau ninamkubali sana msanii huyu hasa katika kipaji chake cha
kuigiza katika hali ya uhalisia wa maudhui ya kidini na kweli
amefanikiwa kuvaa uchungaji wa kweli ambao ni zaidi ya movie wakati ni
movie tu. Kutokana na kipaji hicho na umakini wa uigizaji wake wadau
wengi tunajua kuwa Myamba ni mchungaji ambaye anakanisa lake, lakini
kumbe sio, yeye ni mwigizaji na muumini wa kawaida tu. Hali hii sis
wadau wa filamu ndio tunatamani kuangalia filamu zenye uhalisia wa namna
hii. Katika kundi hili wasanii kama Dr. Cheni, JB, Wema Sepetu na Shamso Ford
ni baadhi ya waigizaji ambao wanakuwa makini katika katika uigizaji
wao;unaweza kufurahi nao au kulia nao ukifikiri kile kinachochezwa ni
ukweli mtupu, kumbe sio ni filamu tu.
Swali
ninalojiuliza hapa nini ambacho kinakosekana kwa wasanii wengi hata
wale waanzilishi wa Tasnia hii? je tatizo ni nini? Je ni kweli swala la
elimu linachangia kama?
Pastor Myamba alivyoshauri kuwa “ni vyema kupata elimu kwani elimu inakufanya ujiamini juu ya unachokifanya na kwa umakini zaidi”.
Nina
Imani kuwa kusaka maarifa ya namana ya kutengeneza sinema zenye
uhalisia na visa litasaidia sana kuleta ushindani sio tu wa ndani bali
wa limataifa; ikumbukwe kuwa filamu ambazo zinakosa uhalisia zinapunguza
mvuto, na hivyo kuwafanya watazamaji kuishiwa na hamu ya kuziangalia
filamu hizo na kuwakosesha kipato na kuongeza umasikini miongoni mwa
wasanii.
Kama
Gayo alivyowahi kushauri kuwa “Ikiwa tutaendelea kutengeneza filamu
zisizo na weledi, zenye visa vilevile na zenye kusukumwa na wasambazaji
au haja ya kuchuma fedha za haraka tu watu watatuchoka na baadaye soko
litakufa”.
Hivyo
kilio cha elimu kwa wasanii kimekuwa ni kilio cha wadau wengi hapa Gayo
anasisitiza kuwa “Pia wasanii na watendaji wengine wanapaswa kupatiwa
mafunzo, kwangu mafunzo ndiyo kitu cha kwanza muhimu kwa mtu yeyote yule
katika kumuongezea stadi zake za utendaji. Kwa jumla kuna upungufu
mkubwa wa mafunzo ya fani mbalimbali za sanaa, ikiwemo filamu. Wasanii
wengi wanajifunza kwa kuiga wenzao. Ingawa hii ni moja ya njia za
kujifunza, tatizo lake ni kuwa huchukua muda mrefu na haina hakika kama
kinachoigwa ni sahihi au la”.
Je ni kweli sekta hii ni ya watu ambao hawajasoma? Mimi ninasema hapana?
Isipokuwa ni sekta ambayo wahusika wake baada ya kushika pesa kidogo
hunogewa na hawataki kujiendeleza kwa kujipanua katika elimu ya
uigizaji; na kwa hiyo ufanisi wa kazi umekuwa wa chini mno.
Msanii Myamba
ametuletea changamoto nzuri ya kuanzisha chuo cha filamu Tanzania
kuppitia chuo hiki wasanii wataweza kukabiliana na changamoto za uandaji
wa filamu kwa wasanii kukubali kujiongezea ujuzi na masilahi bora.Kwa
hiyo eneo hili la mafunzo linahitaji msukumo siyo tu wa kuongeza nafasi
bali pia ubora wake.
Wazungu na kiingereza chao wanasema "Knowledge" comes from getting educated.
"Experience" comes from real life encounters. There is a famous saying that says.
"Experience is better than knowledge!" and "Experience is the Best Education In Life."
Experience and knowledge go hand in hand.
Knowledge is important, because it makes you aware of what is around you. Knowledge also enables a person to become wealthy.
The
more knowledge we have, the more advanced we can become. Education can
give you a good job and assure you a secure future. The world needs
knowledge to discover new things to help everyon
0 comments:
Post a Comment