Home » »

Imani .....Party 2


Ndugu mpendwa nakukaribisha sana katika mfululizo huu wa makala ya Imani;naamini unazidi kubarikiwa na somo hili.Ni mimi Docta Lightness William Ng’unda karibu tuendelee.
       Makala yaliyopita tulizungumza juu ya imani inayoambatana na matendo, na leo nitaendeleza hapohapo ili nisikuache.Imani ya matendo inaenda pia sambamba na ukiri wetu na ni muhimu kuchunguza sana ukiri wetu sio kwa kinywa tu bali katika matendo pia.Ukiri wa matendo huwa una nguvu hata kuliko ukiri wa maneno.Namaanisha usiishie kusema tu bali weka hayo maneno kwa matendo pia.Ni muhimu ukiri wa maneno uende sambamba na ukiri wa matendo.
      Mfano mzuri ni huu watoto wengi wa Mungu wamekuwa wanaishi maisha ya kutozingatia kazi,na wanapendelea maisha ya mteremko kwa watu wengine huku wakidai wanaishi kwa IMANI.Mungu anashindwa kuwabariki kwa sababu hakuna wanachokifanya,wanaishia kumlaumu Mungu na kumwona Mungu kama muongo na kumbe sivyo ilivyo.Mungu ameweka wazi katika (2Wathesalonike3:10) Asiyefanya kazi na asile.Lazima uweke mikakati yako kiroho,kinafsi,kiakili na kimwili kupitia ahadi za Mungu ili afanikishe mipango yako. Ukiomba pesa fanya kazi fulani ili Mungu atumie huo mlango kukubariki huku ukiamini.
IMANI NI MKONO WA KUPOKEA MAJIBU
     Watoto wengi wa Mungu ni waombaji wazuri lakini sio wapokeaji wazuri.Namaanisha mtu anaweza funga hata siku 21 akiomba tu lakini upande wa upokeaji hayupo wala haelewi.Maombi ni mazuri sana ila usiwe unajitesa bure lazima ujue kupokea pia.Inawezekana mambo unayopitia Mungu alishayajibu siku nyingi lakini hukujua jinsi ya kupokea na ndio maana biblia inasema  (Hosea 4:6) watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa).Nguvu ile ile uliyoitumia kuomba itumie nguvu hiyohiyo kupokea.Namaanisha ukijua umeomba jambo lolote sawasawa na mapenzi ya Mungu hilo ni lako tayari, na kujua kwamba ni mapenzi ya Mungu utaangalia neno lake linasema nini juu ya hilo jambo unaloliomba na hayo ndiyo mapenzi ya Mungu.Na huu ndio ujasiri tulio nao  kwake,ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,  atatusikia.Na kama tukijua kwamba atusikia,tuombacho chote,twajua kwamba TUNAZO zile haja tulizomwomba.’(1 Yohana 5:14) Hapa inamaanisha nini? tunajua tunazo zile haja, kwa hiyo ukiomba uwe na ujasiri kuwa tayari unazo haja unazoziomba kwa njia ya imani.
USHUHUDA WANGU
    Rafiki najua shuhuda zinajenga sana na zinainua sana imani ya mtu,mimi nina shuhuda nyingi sana ila ni kwa nia ya kukujenga ili ujenge shauku ndani yako na Mungu atafanya zaidi.Nilikuwa natamani sana kuwa lecture/mwalimu wa chuo kikuu.Na nilipomaliza elimu yangu ya udactari ya chuo kikuu niliomba nafasi ya kuwa mwalimu katika chuo nilichosomea.Tulifanya interview na nilikosa ile nafasi, binafsi iliniuma sana  lakini kwa sababu sikuwahi kuwa na uzoefu wa kufundisha,na katika interview wenye uzoefu walikuwepo hivyo wakachukuwa wenye uzoefu mimi nikakosa.Nikamuuliza Mungu akaniambia umeomba sana anza kuamini kuwa wewe ni lecture nikaanza kukiri ingawa ilikuwa ngumu sababu Tanzania kuna chuo kimoja tu cha kazi niliyosomea ya walemavu,ikabidi nitafute kazi nchi za ulaya na Asia kwa vile walitangaza ajira pia.Siku moja baada ya kuendelea kuamini niliitwa chuo hichohicho nikaambiwa wiki inayofwata nije kazini na nilikuwa napenda sana kuanza kufaya kazi Tanzania na Mungu akanijibu haja ya moyo wangu, na sasa ni lectuere.Usiogope hata wewe mpendwa Mungu aliyetenda kwangu namsii atende na kwako pia ili aufariji moyo wako.Usiogope Mungu anajua kilichobora kwa ajili yako maadamu Bwana ni mchungaji wetu hatutapungukiwa na kitu (ZABURI 23:1) halleluya.Mungu ametuumba tutawale dunia nchi na vyote vijazavyo ni mali ya bwana dunia na wote wakaao ndani yake (Zaburi 24:1),inamaanisha kazi zote pia ni mali yake na anajua wapi atakuweka na kwa wakati gani rafiki.
       Nimesema tena imani ni mikono ya kupokea mahitaji na haja zetu tunazoomba.Tunapokea kwa kadiri ya nguvu itendayokazi ndani yetu yaani imani yetu.Inamaanisha imani yako ikiwa na viwango fulani unapokea haraka zaidi kinachotofautisha majibu mengi ya wana wa Mungu ni imani waliyonayo kwa Mungu juu ya hilo jambo.Kila mtu alipookoka alipewa kiwango cha imani sawa na mwenzake lakini huwa imani inakuwa kulingana na unavyoifanyiza mazoezi ya kuiweka kwa matendo, na hapo ndipo tunapotofautiana sisi kwa sisi.Na imani yako ikikaa bila matendo kuna mda itakufa kama bibilia inavyosema (Yakobo 2:18) lakini mtu akisema, wewe unayo imani ,nami ninayo matendo.Nionyeshe imani yako pasipo matendo,nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo.Mstari wa 26 maana kama vile mwili pasipo roho umekufa,hivyohivyo na imani pasipo matendo imekufa.
        Ni kwa kadiri ya uhakika wa neno la Mungu uliondani yako yaani imani yako ndiyo utapokea na ndiyo maana huwa nasisitizia sana watu wawe wasomaji wa neno ili waongeze uhakika wa mambo yao katika kuzijua ahadi zao na shetani hatakuweza kwa jana la Yesu.Embu fikiria  kuhusu hali unayopta ni kweli hauna uhakia wa neno la Mungu juu ya hali hiyo? Kuna nini Mungu amesema juu ya hali hiyo kwenye neno lake? Anasema (1Petro 5:7) Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. Dai haki yako kwa baba yako maana wewe ni mwana wake na si mtumwa tena.Mungu si mwnadamu hata aseme uwongo ahadi zae zinasimamaa hata nyota zingezimika ahadi zake zadumu hata milele Haleluya.
          Imani ni kuwa na uhakika /ujasiri na udhibitisho moyoni ukisoma tafsiri mbalimbali za kiyunani.Unapoomba ule uhakika wa haja zako kwamba Mungu atakujibu na ujasiri ndio mikono ya kupokea.Ninamaanisha unapokuwa na imani mambo yatarajiwayo yanakuwa wazi au halisi kwako na ndani yako kabla hayajathihirika, nikimaanisha unaanza kuona majibu yako kwa macho ya imani.
         Hivyo imani kama mikono inaambatana na ujasi ili upokee nitafafanua zaidi hapa na kwa mifano ili uelewe zaidi.Kuna kipindi nilikutana na hali fulani nilipoanza kazi,Mungu aliambia nikianza kazi nimpatie mshahara wangu wa kwanza kama malimbuko.Na hata wazazi wangu na marafii walikuwa wananiambia kumbuka mshahara wa kwanza sio wako Lightness.Nilipokuwa nawaza nitaishi vipi mwezi mzima Mungu akanipa wazo la kuanzisha biashara kwa mtaji wa sh alfu 10 tu.Nilikuwaga muoga sana wa kufanya biashara nikawa nikitoka kazini nauza hereni,  mikufu na bangili za wanawake kwa rafiki zangu maofisini na kanisani.Nikaanza kupata hela nyingi sana  hadi mtaji ukafika laki moja na kuendelea, na mpaka sasa najisikia raha sana kufanya biashara na nimeweza hadi kuajiri watu wasiokuwa na kazi nafanya nao na nawalipa.Nitumia ujasiri na Mungu ananibariki sana na sijawahi kupungukiwa au kujuta naipenda kazi yangu na mshahara sasa ni kama mtaji wangu
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog