Home » » BONDIA MAARUFU NCHINI AMTAKA ASKOFU KAKOBE KATIKA ULINGO WA NGUMI

BONDIA MAARUFU NCHINI AMTAKA ASKOFU KAKOBE KATIKA ULINGO WA NGUMI

bondia francis cheka katika pozi
Novemba 9, 1996 mabondia wawili wa Kimarekani wa uzito wa juu waliokuwa na majina  makubwa ulimwenguni Evander Holyfield  na Make Tyson, walisababisha kuibuka hisia za udini katika pambano  lao na hivyo waliwagawa wapenzi wa ngumi katika makundi mawili ya Kikristo na Kiislamu, kufuatia Tyson kuamua kusilimu na kujitangaza kuwa mfuasi wa dini hiyo  kupitia Allah na Mjumbe wake Mtume Muhammad (SAW).

Wakati wa pambano lao lililofanyika katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena ulioko Jijini Las Vagas Jimboni Nevada nchini Marekani bondia Holyfield aliyejitangaza kuwa mlokole anayemuamini Mungu Yehova kupitia mwanaye Yesu Kristo, aliingia ulingoni huku amevali vazi lenye ujumbe unaotoka katika kitabu cha Wafilipi 4:13, akitamba kumsambaratisha vibaya Tyson ambaye alikuwa na sifa ya kushinda mapambano yote, ambapo alifanikiwa kumpiga vibaya mwishoni mwa round ya 10.
Kabla na  baada ya kupigana na Tyson na kumshinda kwa kishindo, alipohojiwa na Vyombo vya Habari Holyfiel alinukuliwa akisema kwa msisitizo kwamba alikuwa na uhakika wa kushinda kutokana na Roho Mtakatifu kumhakikishia hilo.
Bondia Tyson alisambaratishwa ulingoni  na Mlokole Holyfield katika round hiyo ya 10 ya pambano lililogubikwa na hisia za kidini, ikiwa ni muda mfupi  baada ya kusilimu, ambapo umaarufu wake ulishuka  vibaya  na kujikuta akipoteza takribani mapambano yote yaliyofuata hadi alipostaafu ngumi.
Pambano hilo hadi leo lilimecha utafsiri kwamba siku zote  anayemuamini Yesu ni mshindi na kwamba wakati mwingine Mungu Yehova anaweza kuonesha ukuu wake katika njia ambazo binadamu anaweza kuona kama vile zina utata,  lakini bado akaendelea kuitwa Mungu mwenye haki na rehema.


 Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog