Home » »

JOYOUS WAINGIA STUDIO HAPO JANA, NQUBEKO NA MKEWE NAO WAKO TAYARI NA TOUR YAO

Kundi la Joyous Celebration hapo jana lilikuwa kwenye kipindi cha gospel time kinachorushwa na runinga ya SABC2 ya nchini Afrika ya kusini, ambapo kundi hilo likiwa na timu nzima ya waimbaji na wanamuziki wao waliweza kufanya vyema kama ilivyokawaida na kuwabariki watu waliokuwa studioni hapo na wale waliotazama moja kwa moja kupitia runinga huku wakihojiwa na malkia wa muziki wa gospel barani Afrika Rebecca Malope.

Hii si mara ya kwanza kwa kundi hilo kualikwa katika mahojiano pamoja na kuimba kupitia vipindi mbalimbali vya runinga na radio nchini humo, Pia ni kundi ambalo limepitia wakati mgumu wakati likianza kuvuma nchini humo ambapo maneno mabaya yalikuwa yakisemwa kuhusiana na kundi hilo pamoja na waimbaji kwa ujumla hali ambayo kwa namna nyingine imelifanya kundi hilo kusimama na kusonga mbele.


HAPA UNAWEZA KUTAZAMA BAADHI YA PICHA WAKIWA STUDIONI ASUBUHI JANA
Zodwa Mahlangu pamoja na Rebecca Malope kwa chini yake wakifuatilia jambo.
Waimbaji wa Joyous wakiwa studioni jana.
Mkhululi akiwa katika pozi na Charisma ndani ya SABC2 jana.
Kati ya sura mpya ndani ya Joyous Celebration katika pozi.


Wakati hayo yakijiri kwa upande wa Joyous, waimbaji wao waliojitoa kundini baada ya kumaliza mkataba wao Nqubeko na mkewe Ntokozo Mbambo Mbatha wanatarajia kufanya tour yao ya muziki ikiwa ni pamoja na darasa la muziki kwa wanaotaka kupigwa msasa katika tasnia ya muziki nchini humo.

Tour yao inatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao tarehe 31 August katika ukumbi wa Imbizo Conference Centre Empangeni, hii itakuwa furaha kwa mashabiki na wapenzi wa wanamuziki hao kutokana na tour hiyo kufanyika baada ya awali iliyopangwa kufanyika mwezi uliopita kuahirishwa.

Pamoja na hayo pia DVD ya Ntokozo Mbambo iitwayo ''FILLED ALBUM'' aliyoirekodi mwezi wa pili mwaka huu inatarajiwa kuanza kuuzwa mwezi ujao hali ambayo mashabiki wao wamepokea kwafuraha taarifa hiyo.

                             

Nqubeko na mkewe Ntokozo katika pozi.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog