![]() |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
|
![]() |
TAARIFA YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NDUGU
KAILIMA RAMADHANI KUHUSU UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI UTAKAOFANYIKA TAREHE 15
NOVEMBA, 2015 KATIKA JIMBO MOJA NA KATA 25
Ndugu Wananchi
Kama mnavyofahamu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa ya kuahirishwa kwa uchaguzi katika
majibo nane (8) na Kata thelathini na
nne (34). Sababu ya kuahirishwa uchaguzi katika Majimbo na Kata hizo kulitokana
na vifo kwa wagombea katika Majimbo sita na majimbo mengine mawili
yaliahirishwa kutokana na hitilafu mbalimbali.
Kesho tarehe 15
Novemba, 2015 ni Siku ya Kupiga kura ya kuchagua Mbunge katika Jimbo moja na
kuchagua Diwani katika Kata 25.
Jimbo na Kata
hizo ni kama inavyoonekana katika Jedwali hapa chini:#
Jedwali Na.1: JIMBO LINALOFANYA UCHAGUZI WA MBUNGE
TAREHE 15.11.2015
|
NA
|
MKOA
|
HALMASHAURI
|
JIMBO
|
|
1.
|
Lindi
|
Masasi DC
|
Lulindi
|
|
|
|
|
|
Jedwali Na.1: KATA ZINAZOFANYA UCHAGUZI WA DIWANI
TAREHE 15.11.2015
|
NA
|
MKOA
|
HALMASHAURI
|
NA
|
KATA
|
|
1.
|
Geita
|
Geita DC
|
1
|
Ludete
|
|
Mbogwe DC
|
2.
|
Isebya
|
||
|
2.
|
Tabors
|
Urambo DC
|
3.
|
Kiloleni
|
|
Nzega DC
|
4.
|
Mizibaziba
|
||
|
5.
|
Tongi
|
|||
|
3.
|
Arusha
|
Ngorongoro DC
|
6.
|
Malambo
|
|
7.
|
Ngaresero
|
|||
|
4.
|
Mara
|
Rorya DC
|
8.
|
Bakula
|
|
5.
|
Mwanza
|
Kwimba DC
|
9.
|
Bupamwa
|
|
6.
|
Mbeya
|
Chunya DC
|
10.
|
Mwambani
|
|
11.
|
Itewe
|
|||
|
12.
|
Mkola
|
|||
|
13.
|
Mbuyuni
|
|||
|
Mbarali DC
|
14.
|
Rujewa
|
||
|
7.
|
Simiyu
|
Bariadi DC
|
15.
|
Matongo
|
|
8.
|
Tanga
|
Korogwe TC
|
16.
|
Majengo
|
|
9.
|
Tanga
|
Kilindi DC
|
17.
|
Songwe
|
|
10.
|
Njombe
|
Ludewa DC
|
18.
|
Mkongobaki
|
|
11.
|
Ruvuma
|
Madaba DC
|
19.
|
Mahanje
|
|
Namtumbo
|
20.
|
Mkongo Gulioni
|
||
|
21.
|
Lisimonji
|
|||
|
12.
|
Kigoma
|
Kigoma Ujiji
|
22.
|
Kagera
|
|
13.
|
Rukwa
|
Sumbawanga DC
|
23.
|
Milepa
|
|
14.
|
Katavi
|
Mpanda DC
|
24.
|
Magamba
|
|
15.
|
Dar es Salaam
|
Kinondoni MC
|
25.
|
Saranga
|
Aidha, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nawapongeza wananchi
wote katika Jimbo na Kata zinazofanya Uchaguzi kesho kutokana na utulivu waliouonyesha
katika kipindi chote cha kusubili siku ya kupiga Kura kuchagua Mbunge au Diwani
wao.
Ndugu Wananchi
Natoa rai kwa wale wote mliojiandikisha kama Wapiga Kura katuka Jimbo
na Kata zinazofanya Uchaguzi kesho tarehe 15 Novemba, 2015 kujitokeza kwenye
vituo walikojiandikisha ili kuweza kupiga kura na kuwachagua viongozi
wanaowataka bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi. Kura ni haki yako na ni kwa
mustakabali wako na nchi yetu.
Ndugu Wananchi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwakumbusha Wapiga Kura
wote mambo yafuatayo:-
(i)
Vituo
vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni. Iwapo wakati wa
kufunga Kituo watakuwepo Wapiga Kura katika mstari ambao wamefika kabla ya
wakati wa kufunga Kituo na hawajapiga Kura, hao wataruhusiwa Kupiga Kura. Mtu
yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa Wapiga Kura baada ya saa kumi
(10:00) jioni.
(ii) Mpiga Kura akumbuke kubeba Kadi yake ya Mpiga
Kura.
Sheria
inaelekeza kuwa ili Mpiga Kura aruhusiwe kupiga kura ni lazima awe na kadi ya
kupigia Kura. Fomu Na. 17 sio mbadala wa Kadi ya Mpiga Kura. Fomu hii ni kwa
ajili ya Mpiga Kura mwenye Kadi ya Mpiga Kura kutoa Tamko kuthibitisha ndiye
mwenye jina linaloonekana kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kwamba
bado hajapiga kura katika kituo hicho au mahali pengine.
(iii)
Kipaumbele
kitatolewa kwa wagonjwa, wanaoishi na ulemavu wa aina mbalimbali, wanawake
wajawazito au wenye watoto wachanga na wazee ambao hawatatakiwa kujipanga
kwenye mstari.
(iv)
Wakati wote wa
Kupiga Kura na Kuhesabu Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa wawepo kwenye Vituo.
Wajibu wao ni kulinda maslahi ya Vyama vyao na Wagombea. Hata hivyo hawatakiwi
kuingilia masuala ya utendaji ambayo yamekabidhiwa kwa Msimamizi wa Kituo.
(v)
Kura
zitahesabiwa katika Kituo cha Kupigia Kura mara tu Upigaji Kura
utakapokamilika. Baada ya Kura kuhesabiwa, Matokeo yatajazwa kwenye Fomu za
Matokeo ya Uchaguzi, 21B kwa uchaguzi wa Mbunge na 21C kwa Kata zinazofanya
Uchaguzi wa Diwani. Fomu hizo zitatiwa saini na Msimamizi wa Kituo na Mawakala.
Kila Wakala atapewa nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge na Madiwani
na nakala nyingine zitabandikwa mahali pa wazi nje ya Kituo.
(vi)
Msimamizi wa
Kituo/Msimamizi Msaidizi wa Kituo atapeleka Fomu za Matokeo ya Uchaguzi na
vifaa vingine vilivyotumika kwenye zoezi la Upigaji Kura kwa Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi. Wakala wa kila Chama na mlinzi wa Kituo watakaokuwa
popote msafara unapoanzia wataruhusiwa kusindikiza msafara wa kupeleka matokeo
ya Uchaguzi kwenda kwa Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa
Kata.
(vii) Matokeo yote yakishapokelewa na Msimamizi wa
Uchaguzi kwa upande wa Uchaguzi wa Wabunge na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
kwa upande wa Uchaguzi wa Udiwani, yatajumlishwa mbele ya Mawakala na wote wanaoruhusiwa
kuingia kwenye vituo vya Kujumlishia Kura.
(viii)
Kama ilivyokuwa
wakati wa kuhesabu Kura, baada ya ujumlishaji kukamilika, Fomu Na. 24B Kwa
Ubunge na 24C kwa Udiwani za Matokeo ya
Uchaguzi zitatiwa saini na Msimamizi wa Uchaguzi na Mawakala watakaokuwepo.
Mawakala watapewa Nakala za Fomu za Matokeo na Nakala moja moja itawekwa mahali
pa wazi nje ya Kituo cha Kujumlisha Kura.
(ix)
Matokeo ya
Uchaguzi wa Mbunge yatatangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo mara tu baada
ya kazi ya kujumlisha Kura kukamilika.
(x)
Matokeo ya
Uchaguzi wa Diwani yatatangazwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya mara
tu baada ya kazi ya kujumlisha Kura kukamilika.
(xi)
Tume pekee ndiyo
yenye mamlaka Kisheria ya kumtangaza Mshindi wa Kiti cha Ubunge na Kiti cha
Diwani kupitia Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi
Ngazi ya Kata.
Ndugu Wananchi
Tume inapenda kusisitiza mambo muhimu yafuatayo:-
(i)
Mawakala wa
Vyama vya Siasa wanaruhusiwa kuwepo Vituoni
kwa mujibu wa
Sheria na kanuni, Wakala asiyekuwa na barua ya utambulisho kutoka kwa Msimamizi
wa Uchaguzi hataruhusiwa kuingia katika kituo cha kupigia, kuhesabia na
kujumlishia Kura.
(ii) Vyama vyote vya Siasa vinavyoshiriki katika
Uchaguzi vinatakiwa kuhakikisha kwamba vinaweka Mawakala wake katika vituo
vyote vya Kupigia Kura na Kujumlisha Kura. Mawakala hao watatakiwa kuzingatia
Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
(iii)
Mara baada ya
Kupiga Kura na kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi ya 2015 yaliyokubaliwa na
Vyama vyote vya Siasa na kuridhiwa na Mahakama, Wapiga Kura wanatakiwa kuondoka
Vituoni na kuendelea na shughuli zao. Vituoni Vyama vya Siasa vimeweka Mawakala
wake ambao watalinda maslahi ya Vyama husika na Wagombea wao.
(iv)
Mpiga Kura
atapiga Kura kwenye Kituo alichojiandikisha au alichopangiwa na Tume ya Taifa
ya Uchaguzi.
(v)
Watu waliotajwa
kwenye Sheria ndiyo pekee wanaoruhusiwa kuingia kwenye Vituo vya Kupigia, kuhesabia
na kujumlishia Kura.
(vi)
Mpiga Kura
anayeishi na ulemavu wa kutoona ataruhusiwa kuja kituoni na mtu anayemchagua mwenyewe.
Aidha, kwa Wapiga Kura wa aina hii ambao watataka Kupiga Kura zao wao wenyewe
watapatiwa kifaa maalum cha Nukta
Nundu (Tactile Ballot Folder). Vifaa hivyo vitakuwepo katika vituo vyote vya
kupigia Kura.
(vii)
Ni kosa la jinai Mpiga Kura Kupiga Kura zaidi
ya mara moja.
(viii)
Mpiga Kura
ambaye atakuwa na kadi ya Mpiga Kura ila namba ya Kadi yake ni tofauti na namba
iliyo kwenye Daftari la Kituo ataruhusiwa
kupiga Kura.
(ix)
Wapiga Kura
ambao picha zao hazionekani vizuri au hazionekani kabisa kwenye Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura wataruhusiwa
kupiga Kura.
(x)
Wapiga
Kura walioandikishwa na Tume na wanaishi katika maeneo mapya ya kiutawala
yaliyogawanywa wakati au baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika, hivyo,
majina ya maeneo hayo kutofautiana na majina yaliyopo kwenye kadi zao wataruhusiwa Kupiga Kura.
(xi)
Wapiga Kura
ambao wana Kadi za Kupigia Kura na majina yao hayapo katika Daftari la Kituo
walichojiandikishia lakini yapo katika Orodha ya majina ambayo haina picha iliyotolewa
na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wataruhusiwa
Kupiga Kura.
(xii) Kwa mujibu wa Sheria, Mpiga Kura ni lazima awe na
kadi ya kupigia Kura ndiyo aruhusiwe kupiga kura. Hivyo, Mpiga kura asiye na
Kadi ya Kupigia Kura hataruhusiwa kupiga
Kura.
(xiii)
Wapiga Kura
ambao wana kadi ya kupigia kura, lakini hawamo katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kituoni Hawataruhusiwa
kupiga Kura.
(xiv)
Ni marufuku, na
ni kosa la jinai kumkataza mtu kwenda Kupiga Kura.
(xv)
Katika Uchaguzi
wa Mbunge mwenye mamlaka ya kumtangaza Mshindi ni Msimamizi wa Uchaguzi. Kwa Uchaguzi
wa Madiwani mwenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Ndugu Wananchi,
Kwa kumalizia, Tume inawasihi tena Wapiga Kura wote kwenye maeneo
yanayopiga kura kesho tarehe 15 Novemba, 2015 kujitokeza kwa wingi Kupiga Kura
ili kuwachagua Viongozi mnaowataka wawaongoze kwa miaka mitano ijayo.
Tume inapenda kuwahakikishia Wananchi wote kwamba kutakuwa
na ulinzi wa kutosha katika Vituo vya Kupigia Kura.
Ni matumaini ya Tume kuwa hali ya Amani na Utulivu ambayo
imekuwepo wakwati wa uchaguzi tarehe 25 Oktoba, itaendelea kudumishwa ili
kuhakikisha kwamba Uchaguzi unafanyika kwa Utulivu na Amani kwa Ustawi wa Taifa
letu. Kila Mwananchi, Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa tushirikiane wote ili
kuhakikisha kuwa viashiria vya uvunjifu wa Amani na Utulivu vinaepukwa katika
hali ya Amani na Utulivu, Uchaguzi utakaofanyika utakuwa Huru, Wazi na wa Haki.
KUMBUKA KUPIGA KURA NI HAKI YAKO YA MSINGI NA
MUSTAKABALI WA NCHI NENDA KAPIGE KURA.
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA




0 comments:
Post a Comment