Home » » HIKI NDICHO KILICHOTOKEA BUNGENI LEO NA KUFANYA : Wabunge Wa UKAWA Watoke Nje ya Bunge

HIKI NDICHO KILICHOTOKEA BUNGENI LEO NA KUFANYA : Wabunge Wa UKAWA Watoke Nje ya Bunge

Wabunge  wanaounga  umoja  wa  Katiba  Ya  Wananchi, UKAWA  wametolewa  nje  ya  ukumbi  wa bunge  muda  huu  baada  ya  kugoma  kutambua  ujio  wa  Dr Shein bungeni  na  kuanza  kuzomea  huku  wakisema  Maalim Seif....Maalim Seif
 
Wabunge hao awali walitoa msimamo wao wa kutokubali Dk Ali Shein kuhudhuria Bunge hilo wakati rais atakapoingia Bungeni kulihutubia Bunge kwa kuwa hawamtambui kama rais wa Zanzibar kwani kwa mujibu wa Katiba muda wake umekwisha.

Kelele za zomeazomea ziliibuka ghafla wakati Rais  Dk Shein alipoingia bungeni hali iliyoondoa utulivu wa Bunge.

Hata hivyo, Mbunge pekee wa upinzani, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) alibaki ndani ya Bunge kwa utulivu na kuendelea kusikiliza hotuba ya Rais.

Awali, wabunge hao walimuandikia barua Spika wa Bunge wakihoji uhalali wa hotuba ya Rais bungeni endapo Dk Shein atahudhuria Bunge hilo kama Rais wa Zanzibar.

Ukawa wameendelea kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (NEC) kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais wa Zanzibar, huku mgombea wa CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akidai kuwa ameshinda kutokana na kura halali alizokusanya kwenye vituo vyote. 

Spika  wa  bunge,Job Ndugai  aliwataka  wabunge  hao waache kuzomea  na  badala  yake  wakae chini  lakini  wakakaida, hali  iliyomfanya  awaamuru  watoke  nje kwa  hiari  yao  kabla  nguvu  ya  dola  haijatumika  kuwatoa.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog