Home » » Mengine kutoka Mahakamani baada ya CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa kiongozi wao Mwanza.. (+Picha)

Mengine kutoka Mahakamani baada ya CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa kiongozi wao Mwanza.. (+Picha)


Kulikuwa na stori zikichukua nafasi kila siku kwenye vyombo vya habari kuhusu ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita, Alphonce Mawazo.
Charles Mkumbo
Kamanda wa Polisi Mwanza, Charles Mkumbo
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo siku chache zilizopita iliagiza kwamba kusiwepo shughuli za kuaga mwili wa marehemu huyo kutokana na ishu ya kipindupindu kilichoibuka maeneo mbalimbali ikiwemo ndani ya Mwanza yenyewe.
index v
Viongozi mbalimbali wa CHADEMA ikiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa Chama hicho, John Mallya wamefika Mahakama Kuu Mwanza na kesi tayari imesomwa.
index vi
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe akiwa nje ya Mahakama Mwanza.
Sentensi za Mwanasheria wa CHADEMA, John Mallya hizi hapa baada ya kutoka nje ya Mahakama >>> “Leo tumefungua kesi ya madai Mahakama kuu kwa hati ya dharura, mlalamikaji wa kesi ni baba mdogo wa marehemu Mawazo… Maombi yetu ni kupata ruhusa ya Mahakama ili kutengua zuio la Mkuu wa Polisi Mwanza kuhusu kuaga mwili wa marehemu Mawazo.”- John Mallya, Mwanasheria wa CHADEMA.
index ii
John Mallya akiwa nje ya Mahakama.
Sentensi nyingine za John Mallya ana haya >>> “Kuna Mawakili watatu, kesi imesikilizwa leo upande mmoja na upande wa pili wa RPC Mwanza na Mwanasheria wa Serikali watasikilizwa kesho asubuhi… Jaji ameona jambo hili ni la dharura na linahusu mwili wa mtu aliyekaa mochwari kwa zaidi ya siku nane, amesema ataifanya kwa haraka.”-
index iv
Kuhusu mwendelezo wa kesi hiyo, Mahakama itaendelea nayo kesho Jumanne November 23 2015 na hiki ndio alichokisema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe >> “Tumefungua madai ya kutaka kumuaga Kamanda wetu Mawazo, madai yetu yamepokelewa  Mahakama kuu, yamepangiwa Jaji na kesho asubuhi suala letu litaanza kusikilizwa” >>>
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog