Home » » Unategemea kupokea kadi za Christmas na mwaka mpya 2015 ?! Ikulu TZ imeamua haya..

Unategemea kupokea kadi za Christmas na mwaka mpya 2015 ?! Ikulu TZ imeamua haya..

Serikali imeendelea na msimamo wake wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, baada ya Rais Magufuli kuondoa safari za nje, mamilioni ya pesa kuokolewa katika uzinduzi wa Bunge sasa imepiga marufuku uchapishaji wa kadi za sikukuu ya Christmas na mwaka mpya.
Katika taarifa yake Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christmas na mwaka mpya kwa gharama za Serikali mwaka huu.
Balozi Sefue ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo afanye kwa gharama zake mwenyewe.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa imesema fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji wa uchapishaji wa kadi hizo zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananchi waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog