Home » » Kipigo cha Madrid cha 4-0, Barcelona wamekiamishia kwa Real Sociedad, Full Time ya LALIGA Nov 28 (+Pichaz&Video)

Kipigo cha Madrid cha 4-0, Barcelona wamekiamishia kwa Real Sociedad, Full Time ya LALIGA Nov 28 (+Pichaz&Video)


Mtu wangu wa nguvu November 28 zilipigwa mechi kadhaa kali barani Ulaya ila kwa upande wa Ligi Kuu Hispania mchezo wa kwanza kupigwa November 28 ulikuwa ni mchezo wa FC Barcelona ambao walishuka katika dimbani lao na Nou Camp kuikaribisha Real Sociedad iliyokuwa nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania (LALIGA).
Real Madrid 0-2 Barcelona Highlights
Kama ilivyo kawaida yao FC Barcelona waliendelea kuutawala mchezo kwa asilimia kubwa kuzidi Real Sociedad ambao hadi dakika ya 70 walikuwa wana wastani wa asilimia 49 ya kumiliki mpira. FC Barcelona walianza kwa mashambulizi kwani dakika ya 13 Andre Iniesta alipiga kichwa kikagonga mwamba.
2200
Mambo yalianza kuwa mabaya kwa upande wa Real Sociedad baada ya Dani Alves kutoa pasi ya goli na Neymar kupachika goli la kwanza kwa FC Barcelona dakika ya 22, dakika nne kabla ya kwenda mapumziko Dani Alves alitoa pasi ya pili ya goli na Luis Suarez kuiandikia FC Barcelona goli la pili dakika ya 41.
suarez_goal_3512799b
Mchezo uliendelea kuwa mgumu kwa Real Sociedad licha ya kuwa kipindi cha pili waliimarika kiasi na kujitahidi kumiliki mpira kidogo, Neymar dakika ya 53 akapachika goli la tatu na Lionel Messi akaitimisha kwa kufunga goli la nne dakika ya 90 na kufanya mchezo kumalizika kwa ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Real Sociedad. Huu ni mchezo wa pili FC Barcelona kufunga goli 4-0 baada ya weekend iliyopita kumfunga Real Madrid.
Video ya magoli ya FC Barcelona
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog