
Hatimaye mahakama hiyo imefikia uamuzi wa kuisogeza kesi hiyo hadi hapo kesho Novemba 26 ambapo inatarajiwa hukumu kutolewa rasmi.
Millardayo.com ilipata nafasi ya kufanya exclusive interview na wakili wa Chadema John Mallya pamoja na naibu katibu wa Chadema Salum Mwalimu.
Na hapa naibu katibu mkuu anazungumza>>
“Pande zote mbili zimemaliza kuwasilisha hoja zao, imeamuliwa kesho tukutane saa saba, mwenendo unarithisha na ni imani yetu kuwa haki itapatikana”;- Salum Mwalimu
“Hatutarajii baada ya hukumu kutaendelea kutokea tena kwa vitendo kama hivi, lai yetu kama chama na familia ni kwamba tuendelee kutunza amani na utulivu kwakuwa ndio jadi yetu” ;- Salum Mwalimu
“Tunawaomba ndugu na mashabiki wetu waendelee kutunza amani hadi hapo kesho saa 7 tutakapo kuja kupata hatma na tutaelezana utaratibu mpya, na tuendelee kuionyesha dunia kuwa Chadema ni watu wa amani ” ;- Salum Mwalimu

Kwa upande wake mwanasheria wa Chadema John Mallya akayasema haya>> “pande zote mbili zimetoa hoja ya msingi ya kwanini sisi tunaomba maombi yetu na upande wa jamuhuri wametoa yao ya kwanini wao wanaona tusipewe maombi yetu, mabishano yalikuwa makali, mheshimiwa jaji ameenda kuandika hukumu na kesho saa saba tutapata uamuzi wa jaji juu ya jambo hili huku tukiamini haki itatendeka” JOHN MALLYA



Hapa nimekuwekea sauti ya mwanasheria pamoja naibu katibu mkuu Chadema>>>
0 comments:
Post a Comment