Home » » DC Paul Makonda na wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki…kilichoamuliwa ni hiki!!

DC Paul Makonda na wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki…kilichoamuliwa ni hiki!!

Wiki iliyopita wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha urafiki walifanya mgomo kwa madai ya kutolipwa mishahara yao kwa muda mrefu
Leo mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alikutana na wafanyakazi wa kiwanda hicho, Dar es salaam na kufanya mazungumzo nao ikiwa kusikiliza kero zao, kisha kufikia muafaka wa wao kurudi kazini na kuendelea na shughuli kama kawaida.
Amesema atakutana na Rais Dk. John Magufuli ili kuweza kumweleza matatizo ya wananchi wa Wilaya yake na kulitafutia ufumbuzi.
“Nimevunja ratiba zote ili nije kuwasikiliza, nataka kutoa kikomo changu kuanzia tarehe 1 mwezi ujao wakati tunakwenda kula sikukuu za Krismas na mwaka mpya kila mtu awe amelipwa mafao yake, agizo langu la kwanza kwa uongozi kesho wakutane kwenye mahakama husika pamoja na viongozi wenu wa watumishi kwa ajili ya kupitia malipo yenu ili yaweze kufanana” Paul Makonda.
“Nyinyi mtakaporidhika wao waonyeshe utekelezaji umefikia wapi, kitakachokwenda kufanyika kwenye mahakama ni kuoanisha kuwa mnastahili kulipwa? unaweza kukuta umeandikiwa unatakiwa kulipwa elfu 80, iyo elfu 70 inakwenda wapi, lazima mfahamu?..Makonda
Kingine Makonda amewataka viongozi wa kiwanda hicho “ifikapo tarehe 24 mwezi huu uongozi utakapomaliza maamuzi ubandike matangazo jinsi mtakavyolipwa pesa zenu na baada ya kuwa mmelipwa ziko taratibu za kisheria juu ya nani mwenye sifa ya kuwa mwajiriwa wa kudumu, katiba nyingine inatoa mamlaka kwa wafanyakazi, mlilolifanya ni tendo la kikatiba, ni haki yenu ya msingi” Makonda.
Makonda amewaomba wafanyakazi wote waweze kurudi kazini kuendelea na kazi kama kawaida.
DSC_9541
Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog