Home » »

WATU WATATU WAUAWA KWA KUCHARANGWA SIME NA MAPANGA MAPIGANO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA HUKO MOROGORO.


Watu watatu wamefariki dunia wakiwemo wakulima wawili na mfugaji  mmoja na watu sita wamejeruhiwa vibaya kwa kukatwa kwa sime na mapanga kufuatia mapigano yaliozuka kati ya wakulima na wafugaji  katika mbonde la matembele linaunganisha kijiji cha mabwegere na mbigiri wilayani kilosa mkoani Morogoro.


Mkuu wa wilaya ya kilosa Bw Elis Tarimo akizungumzia tukio wakati alipotembelea majeruhi katika hospitali ya mission St Joseph dumila  amesema chanzo cha tukio hilo ni wafugaji wawili waliwahoji  wakulima waliokua katika shughuli za kutayarisha mashamba kuwa   kwanini hawajafuata taratibu za kujisajili na kuomba kibali kutoka serikali ya kijiji.

 Kufuatia hali hiyo wakulima waliwajibu kuwa wameruhusiwa na mkuu wa mkoa walime ndipo wakatoa taarifa kwa kundi la wafugaji  wapatao 60 ambapo yakaanza mapigano kwa kutumia mikuki marungu na sime na mapanga amewataja waliofariki dunia  kuwa ni Joseph Peter (26) mkulima ,Rajabu Selemani (55) mkulima na Kaduru Kashu (30) mfugaji na wengine wamelazwa katika hospitali na mmoja  amehamishiwa katika hospital ya mkoa wa Morogoro.

Kufuatia tukio hilo mkuu wa wilaya yakilosa Bw Elias Tarimo amesema tukio hilo la mauji halita vumilika na lazima vyombo vya sheria vifanye kazi na kuhakikisha watuhumiwa wanakamtwa huku akitupia lawama wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kuchelewa kuleta wasuluhishi wa mgogoro huo kama walivyoahidi ili kuhakiki upya mipaka ya vijiji ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji iliyodumu kwa muda mrefu. 

Nao majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mission St Joseph Dumila wamelalamikia serikali kushindwa kumaliza tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji ambapo wameelezea mapigano yalivyotokea.

 Naye muuguzi wa zamu katika hospitali ya mission St Joseph Melania Shayo amesema wakulima wawili waliofariki dunia wakati wakipatiwa matibu  na kukiri kupokea maiti moja ya mfugaji alieuwawa wakati wa mapigano hayo.

Mapigano haya yamekuja siku chache ambapo nyumba 41 zilichomwa moto zikiwemo za wakulima na wafugaji kufutia mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Mabwegre wilayani kilosa ambapo mkuu wa wilaya aliwakutanisha wakulima na wafugaji kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo hata hivyo mkutano huo uligubigwa na mivutano na wafugaji na kuondoka kabla ya mkutano kumalizika.
via>>ITV
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog