Home » »

Matokeo ya Kidato cha Nne na QT 2014



Ili kuona matokeo ya CSEE, bofya hapa na kwa matokeo ya QT, bofya hapa


Katibu Mtedaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk Charles Msonde ametangaza matokeo ya mitihani ya Shule za Sekondari ya Kidato cha Nne ya mwaka jana na kusema, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013.

Dk Msonde amesema kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 58.25 hadi asilimia 68.33 kumetokana na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN).

Dk Msonde ameishukuru Serikali kwa BRN na Walimu kwa jitihada zilizofanikisha kupatikana kwa matokeo hayo.

Matokeo haya yametolewa kwa kutumia mfumo mpya wa wastani wa pointi badala ya madaraja kama ilivyozoeleka kwa miaka iliyotangulia.

Baraza hilo limewafutia metokeo watahiniwa 128 wa kujigetemea kutoka vituo vya Kisesa mkoani Mwanza na Lubabo huko Zanzibar kutokana na udanganyifu uliokithiri. 
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog