Home » »

BINTI WA MIAKA 27 AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA HUKO SHINYANGA VIJIJINI, WIVU WA KIMAPENZI WAHUSISHWA.


Mwili wa Marehemu Huma Simon ukiwa eneo la tukio
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Huma Simon (27) mkazi wa kitongoji cha Solwa Kata ya Solwa Wilayani Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa Majirani Mwili wa marehemu Huma umekutwa asubuhi katika eneo la Shule ya msingi Solwa ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali na kutelekezwa.

Taarifa zimesema Huma ambaye anaishi na Mama yake Mzazi, alitoka usiku katika chumba alichokua amelala na kumuacha Mtoto wake wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka miwili, na kukutwa asubuhi akiwa ameuawa.

Wananchi wa Kata Solwa wakiutazama Mwili wa Marehemu eneo la Tukio
Aliyebebwa Mgongoni Ndio Mtoto wa Marehemu aliyeachwa na Mama yake akiwa amelala usiku.
Mama Mzazi wa Marehemu akiwa amekaa chini analia mara baada ya kukuta Mwanae akiwa ameuawa
Mwili wa Marehemu Huma ukiwa unachukuliwa na Maafisa wa Polisi
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog