Home » »

Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) Kimemtaka Waziri Sitta Aibane SUMTRA Ipunguze Nauli


CHAMA cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimewaomba Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sita kuingilia kati na kuagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), isikilize kilio cha wananchi kuhusu kupunguzwa kwa nauli.
 
Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti wa chama hicho, Hassan Mchanjama wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam.
 
Alisema wamefikia uamuzi huo baada ya Ewura kushusha bei ya mafuta, hivyo ni vyema na abiria nao wakanufaika kutokana na mafuta kushuka tangu mwaka jana Desemba, kwani inaonekana wanaonufaika ni wamiliki wa vyombo vya usafiri.
 
Aliongeza kuwa imekua ikishuhudiwa mara kwa mara mafuta yakipanda kidogo, nauli nazo zinapanda haraka, lakini mafuta yakishuka Sumatra hawataki kuitisha mkutano na wadau ili kujadili kushusha nauli .
 
“Sisi Chakua tumechukua hatua ya kwanza kuwaandikia barua, lakini Sumatra ipo kimya tukaandika tena Februari 5, lakini bado wamekaa kimya,” alisema Mchanjama.
 
Alisema Chakua inataka nauli zote zipungue kwa asilimia 25, kwa mfano nauli za daladala chini ya kilometa 10 nauli ya sasa ni Sh 400 hivyo ipungue hadi Sh 300 na mikoani nauli ipungue kwa asilimia 25.
 
Alisema nauli ikipungua itasaidia kupunguza bei za bidhaa nyingine ikiwemo vyakula, kwani mfumko wa bei unachangiwa na gharama za usafirishaji.
 
Katibu wa Barabara wa chama hicho, Gervas Rutaguzinda aliitaka serikali kujenga vibanda vya kupumzikia abiria katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, kwani kila abiria anayeingia katika kituo hicho analipa Sh 200.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog