Home » »

BREAKING NEWS..!! BINTI MCHAWI ANASA KWENYE NYUMBA YA MTU AKIWANGA HUKO SHINYANGA.




Siku chache tu baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi mwenye umri wa miaka 80 kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi huku Ndembeza mjini Shinyanga leo binti binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 anayedaiwa kuwa ni mchawi amekutwa kwenye nyumba ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga akiwa amevaa kishirikina huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 Geita,Mwanza na Shinyanga kuwanga katika nyumba hiyo .

Mguu wa binti huyo aliyedai kutoka Ushirombo.

Tukio hili limetokea leo asubuhi katika mtaa wa Bushushu nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake zaidi ya 10 kutoka kanda ya ziwa kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe.

Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakimhoji binti huyo

ambapo baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary Joseph.

Anasema leo ni mara ya tatu wanakuja kufanya uchawi wao,lengo lao ni kutaka ndugu yao aolewe na Massawe,walikuja siku ya kwanza wakakuta mke wa Massawe akisali,wakashindwa,wakarudi mara ya pili kwa ajili ya kusambaratisha ndoa,wakafanikiwa leo walikuja kufanya sherehe kwa kazi hiyo lakini wenzake wamemkimbia-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga. 
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog