Home » »

BABA AKUTWA AMEKUFA KWENYE BWAWA LA MAJI HUO SHINYANGA, MKE ADAI ALITOKA USIKU KUJISAIDIA

.


Mwili wa Marehemu Charles Makima ukitolewa kwenye Maji hayo

Mkazi wa kitongoji cha Nyashimba kijiji cha Solwa, Wilayani Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga, Charles Makima (50-55) amekutwa amekufa maji katika bwawa la Sululuni lililopo katika kijiji hicho.

Mashuhuda wamesema Marehemu Makima amekutwa akielea juu ya maji katika Bwawa hilo jana majira ya saa kumi na moja jioni na ndipo taarifa ilipotolewa kwa wananchi na uongozi wa kijiji kwa ajili ya kuutoa mwili huo ndani ya maji.
Wananchi wa Kijiji cha Solwa Wakiutazama mwili wa Marehemu Charles Makima

Kwamujibu wa mke wa Marehemu ambaye jina lake halijapatikana mara moja, amesema mumewe alitoka usiku wa kuamkia jana kwenda nje kujisaidia lakini hakurudi tena, na walifanya jitihada za kumtafuta bila mafanikio hadi alipokutwa katika bwawa hilo.

Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika lakini imedaiwa kuwa Marehemu Makima alishawahi kufanya jaribio la kujiua kwa kujikata kisu shingoni mnamo mwaka 1984. 

Hata hivyo baada ya Mwili huo kuopelewa na wananchi, umepelekwa nyumbani kwa Marehemu kuhifandhiwa hadi hapo jeshi la polisi litakapofika kwa ajili ya uchunguzi.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog