Home » »

MAUAJI TENA SHINYANGA..!! MWINGINE AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA USIKU WA MANANE AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE.


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha

Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Winfrida Simon (35) ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana akiwa amelala nyumbani kwake katika kijiji cha Manyada, wilayani Shinyanga.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku katika kijiji hicho kilichopo kata ya Usanda.

Kamanda Kamugisha amesema watu hao wamemkata Winfrida mapanga sehemu za kichwani na shingoni hali iliyosababisha kifo chake papo hapo.

Amesema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa na kwamba tayari watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Kamugisha amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Misana Juma(30), Joseph Jahila(24) Emmanuel Joseph(39) na Msafiri Kulwa wote wakazi wa Manyada kata ya Usanda wilayani Shinyanga.

Tukio hilo linatokea ikiwa ni Siku tatu tu baada ya watu watatu kuuawa kwa kukatwa mapanga kisha kufungiwa ndani ya nyumba zaidi ya siku 5 katika kijiji cha Bugogo wilayani Shinyanga.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog