Home » »

BAADA YA GWAJIMA, EMMANUEL MBASHA NAYE AKIKANA KICHANGA KILICHOZALIWA NA FLORA MBASHA.


Familia ya Mbasha inaendelea kutengeneza vichwa vya habari. 
 Baada ya mchungaji maarufu nchini, Gwajima kukanusha kuwa si baba wa mtoto wa Flora Mbasha, mume wa muimbaji huyo wa muziki wa injili, Emmanuel naye amesema hatambui chochote kuhusu kuzaliwa kwa mtoto huyo.
 Mbasha ambaye pia ni muimbaji wa muziki huo amesema ana mtoto mmoja mwenye umri wa miaka kumi na kwamba taarifa za kuwa Flora amejifungua anazisikia kama watu wengine.
“Nina mtoto mmoja, nina mtoto mmoja anaitwa Lizy na kama miaka 10 hivi. Wewe ndo unanieleza mimi kama amejifungua, kama amejifungua ni jambo jema na jambo la kumshukuru Mungu,” Mbasha alikiambia kipindi cha Sunrice cha Times FM.

1 comments:

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog