Home » »

Wafuasi wa CUF Wawazidi Ujanja Polisi Mahakamani.....Kesi yapigwa kalenda hadi March 23


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam,jana iligeuka mithili ya uwanja wa sinema baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwafutia mashitaka watu 30 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kutimua mbio na kutoweka eneo la mahakama hiyo.

Kitendo hicho kiliwafanya wafuasi hao wanusurike kuunganishwa katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, katika mahakama hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, Mawakili wa Serikali, Joseph Maugo na Mwanaamina Kombakono, kudai kuwa DPP amewasilisha hati ya kuwafutia kesi washtakiwa na hivyo, hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Alidai DPP analiondoa shauri hilo chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Sheria za Makosa ya Jinai (CPA).

Hakimu Mchauru alisema kwa kuwa DPP ameona hana nia ya kuendelea kuwashitaki, mahakama yake haina sababu ya kuendeleaa kuwashikilia washtakiwa, hivyo inawaachia huru.

Baada ya washtakiwa hao kuachiwa huru walitoka eneo la mahakama na kutimua mbio wakiwa sambamba na wadhamini wao.

Saa 5:10 asubuhi, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mchauru, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba alipanda kizimbani kusikiliza kesi yake.

Jopo la mawakili wa serikali liliomba mahakama kubadilisha hati ya mashitaka na kuwaunganisha wafuasi 30 pamoja na Profesa Lipumba, wakati huo wakiwa wamekwishaondoka katika eneo la mahakama na kutawanyika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 23, itakapotajwa tena wakati washtakiwa wote wakiwa nje kwa dhamana.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog