Home » »

MWENDESHA PIKIPIKI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KISHA KUPORWA PIKIPIKI YAKE.


Mtu mmoja mikocheni wilayani Mvomero mkoani Morogoro ameuawa kwa kupigwa risasi shingoni na kisha kuporwa pikipiki aina Boxer ambapo jeshi la polisi linawashikilia watu watatu waliohusika na tukio hilo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema jeshi la polisi lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata watu watatu wanasadikiwa kujihusisha na tukio hilo na linaendelea kuwahoji kisha watafikishwa mahakamani.
 
Aidha kamanda Paulo amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa aliye kimbia ambapo katika hatua nyingine wamefanikiwa kumkamata hawara wa mtu huyo aliyejulikana kwa majina ya Husuna Isimaeli mkazi wa mkindo ambaye alikuwa akimhifadhi mtuhumiwa  na jeshi la polisi litaendelea kumshikilia kwa mahojiano ilikumpata mtuhumiwa aliye kimbia.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog