Home » »


MZEE AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA KUACHWA ZIKINING'INIA.



Mkazi wa Kijiji cha Majimaji kilichopo Tunduru mkoani Ruvuma, Patrick Vitus (70), amekatwa sehemu zake za siri na kuachwa zikining’inia.


Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Hussein Mkali, alisema Patrick alikatwa sehemu zake hizo na mpwa wake Zainabu Said (32), baada ya kumkatalia kwenda kumfuata mumewe aliyekuwa kwa mke mdogo.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tisa usiku katika maeneo ya mashamba ya kijiji hicho ambako walikuwa wakifanya shughuli za kilimo.

Alisema mume wa Zainabu ni Musa Said (40), aliyeenda kulala kwa mke mwingine ambaye jina lake halikupatikana na kumsababishia Patrick kukatwa sehemu zake za siri.

Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo, ofisi ya kijiji imemkamata Zainabu na kumpeleka polisi ambako ndiko maelezo zaidi ya kuhusiana na tukio hilo yatatolewa huku Patrick akiwa amepelekwa Hospitali ya Tunduru.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, alisema atatoa ufafanuzi wa tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.
 Na Amon Mtega, Songea
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog