MWALIMU ALIYEISHI NA NDOO ZA KINYESI NDANI, ATOA SIMULIZI YA AJABU... USHIRIKINA WATAJWA. Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini  Dar, Gaudensia Albert. HII ni simulizi ya aibu! Tukio la mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini  Dar, Gaudensia Albert, mkazi wa Kisiwani Kata ya Sandali wilayani Temeke kuishi na vinyesi, mikojo na matapishi chumbani kwake, limeibua mshtuko na aibu ndani yake. Kinyesi kikiwa kwenye ndoo. Kwa mujibu wa mwenye nyumba, Reuben Shayo, mwalimu huyo anayefundisha masomo ya sayansi aligundulika hivi karibuni kuwa anaishi ndani...
BREAKING NEWS..!! KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA. Habari zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kwamba Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), Kapteni mstaafu John Damian Komba amefariki dunia. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Kapteni Komba amefariki katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya sukari yaliyokuwa yakimsumbua. Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) atakumbukwa sana kwa umahiri wa utunzi wa nyimbo mbalimbali za kwaya akiwa na TOT. Miaka mitatu iliyopita, Komba alipelekwa nchini...
Ziko hapa kurasa za mwanzo na mwisho za Magazeti ya leo February 28, 2015 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ....
Mwanaume wa Miaka 45 Ahukumiwa kifungo cha maisha Jela kwa kosa la Kumbaka Mtoto wa Miaka Minne Mwanaume mmoja Yusufu Chatambala (45) mkazi wa Kijiji cha Makutupa Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.   Mwendesha mashtaka wa polisi Godwill Ikema ameiambia mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Feb 20 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Makutupa kilichopo Wilayani Mpwapwa ambapo alimbaka mtoto mdogo...
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KUTEKETEA KWA MOTO KWENYE GARI. Watu watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es Salaam.   Kikosi cha zimamoto walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta kama ilivyozoeleka. Baada ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata...
ZITTO KABWE KUTANGAZA MAAMUZI MAGUMU YA KUJITOA CHADEMA. MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema hatma yake kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) itajulikana katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa. Raia Mwema linafahamu kwamba tangazo hilo la kisiasa linahusu mustakabali wake wa kisiasa ndani ya Chadema, chama ambacho amekitumikia katika maisha yake yote ya kisiasa tangu akiwa mtoto wa umri wa miaka 16. Katika mahojiano aliyofanya kwa njia ya mtandao na gazeti maarufu la Guardian la Uingereza wiki iliyopita, Zitto alisema kuna kitu kikubwa...
Andrew Chenge AGOMA Tena Kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.....Aomba Aruhusiwe kukata Rufaa Mahakama kuu. MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ameendelea kupambana ili Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, lisiendelee kusikiliza shauri lake, licha ya pingamizi lake kutupiliwa mbali jana.   Chenge amewasilisha ombi la kukata rufaa Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi wa baraza hilo, uliotolewa jana na kusomwa na Jaji Hamisi Msumi, ukisema madai yaliyowasilishwa kwenye pingamizi la mbunge huyo, hayalihusu baraza hivyo shauri linapaswa kuendelea...
Mwanamke Auawa na Mumewe Kwa Kipigo na kisha Mwili wake Kufukiwa katika Zizi la Ng'ombe Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuzika mwili wake kwenye boma la ng'ombe.   Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25 mwaka huu saa 11:45 jioni.   Akieleza mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na...
Wafuasi wa CUF Wawazidi Ujanja Polisi Mahakamani.....Kesi yapigwa kalenda hadi March 23 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam,jana iligeuka mithili ya uwanja wa sinema baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwafutia mashitaka watu 30 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kutimua mbio na kutoweka eneo la mahakama hiyo. Kitendo hicho kiliwafanya wafuasi hao wanusurike kuunganishwa katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, katika mahakama hiyo. Tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi baada...
JWTZ Watoa Tamko Baada ya Ajali ya Ndege ya Kivita Iliyotokea Mkoani Mwanza Leo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza. Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake inawaka moto...

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog