Home » » VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UHUSIANO.

VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UHUSIANO.

Mahsusi kwa watu wanaotarajia kuanzisha mahusiano thabiti na yenye malengo pamoja na wale ambao tayari wamo ndani ya mahusiano ya aina hiyo www.mtembezi.com imekuandalia vitu vya kuzingatia karibu twende sawa.

KWA WATARAJIWA

1.Muonekano.Usidanganyike na muonekano wa nje au yale maongezi ya mwanzo. Kila mtu hua mstaarabu siku za mwanzo hata wale ambao hawana ustarabu.

2.Usikimbilie kutangaza nia haraka.Siku zote ni rahisi mtu kua muwazi kwa rafiki yake kuliko kwa mtu ambae anajua anataka mahusiano nae kwa hofu ya kumpoteza.Tumieni muda wakutosha kufahamiana kama marafiki kabla hamjajiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi.

3.Uliza maswali kuhusu vitu ambavyo ni muhimu sana kwako.Unapoanzisha mahusiano mapya inabidi ujue vitu muhimu kutoka kwa mwenza wako.Kwa mfano kama ni mtu wa familia au sio.

4.Penda kujua malengo yake ya baadae.Hii itakuwezesha kugundua ni mtu wa aina gani,kama ni mpenda maendeleo,mtu wa starehe tu n.k.

5.Kuwa muwazi.Hii inakwenda kwa pande zote,kuna vitu ambavyo ukimwambia mtu ni vidogo sana ila ukificha vinakua na kusababisha migongano kwenye mahusiano.

6.Hakikisha uwezo wenu wa kuelewa unaendana.
Hapa siongelei darasa ila mnavyokua sambamba kwenye maongezi ya kawaida tu yasiyo hitaji degree.

7.Onyesha misimamo yako hata kama unaona ni migumu kueleweka. Ni vizuri mtu akikubali, kujiingiza kwenye mahusiano na wewe awe akijua atakua na mtu wa aina gani. Kama hupendi nguo fupi, mwanamke/ mwanaume mnywaji wa pombe, mvuta sigara n.k inabidi mwenza wako ajue ili aanze kujirekebisha mapema ili kuepusha mizozo.

8.Hakikisha kuna vitu mnavyoshabihiana. Kabla ya kuingia kwenye mahusiano inabidi uchunguze vitu ambavyo mnaendana ili kuimarisha ukaribu wenu ili kuepusha kila mtu kwenda na njia yake.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog