Home » » SERIKALI YASISITIZA KUTOA MILIONI 50 KWA KILA KIJIJI

SERIKALI YASISITIZA KUTOA MILIONI 50 KWA KILA KIJIJI

Serikali imesema kuwa baraza la uwezeshaji Wananchi(NEEC),limeanza kutengeneza utaratibu wa namna ya fedha milioni 50 kwa kila kijiji zitakavyoweza kuwafaisha wananchi wote vijijini wakiwemo Vijana na Wanawake.

Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa nchini Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Muhagama, amesema fedha hizo zitatolewa kwa kila Mtanzania bila kujali itikadi ya Vyama kama habari ambazo zinasaambaa sasa kuwa watagawiwa wanachama wa CCM, pekee.jenistaWaziri Muhagama, amesema jambo hilo linalozungumzwa ni hofu tu ya baadhi ya watu na kuongeza kuwa serikali itazingatia utaratibu wa kisheria wa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia Watanzania wote wanaohusika na mpanngo huo.

Mhe. Muhagama amesema kuwa fedha hizo zilikuwa ni ahadi ya rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kampeni zake ambazo zipo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini haimaanishi kuwa fedha hizo zitagawiwa kwa wanachama wa chama hicho Pekee.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog