Home » » UPINZANI WAIPA ‘HEKO’ NEC KWA KUTOA VYETI VYA SHUKRANI

UPINZANI WAIPA ‘HEKO’ NEC KWA KUTOA VYETI VYA SHUKRANI

Vyama vya siasa vya upinzani vimeipongeza tume ya taifa ya uchaguzi kwa hatua yake ya hivi karibuni ya kutoa vyeti vya shukrani kwa vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka jana hapa nchini na kuelezea hatua hiyo ni mwanzo mzuri wa kuaminiana na vyama vya siasa.damian-lubuva_nec2

Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini DAR ES SALAAM,katibu mkuu wa chama cha NRA,HASSAN KISABYA ALMAS,amesema,kitendo hicho kinaonesha ni jinsi gani tume ya taifa ya uchaguzi ilivyobadilika kutoka iilivyokuwa ikifanya mambo yake zamani ambapo ilionekana kutokujali vyama vya upinzani.

Amesema wao kama vyama vya upinzani watajitahidi kushirikiana na tume ya uchaguzi kuimarisha amani iliyopo nchini baada ya uchaguzi katika maisha ya kawaida ya siasa,kutokana na tume yenyewe kuonesha ukomavu kwa namna ilivyosimamia suala la amani na utulivu katika uchaguzi mwaka jana kwa kutopendelea upande wowote.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog