Home » » GARI LAZAMA BAHARINI “KIVUKONI”

GARI LAZAMA BAHARINI “KIVUKONI”

Alfajiri  ya leo gari aina ya Coaster lililokuwa katika foleni ya kuingia katika kivuko upande wa Posta kuelekea Kigamboni lilizama katika Bahari eneo la Kivukoni.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanaeleza chanzo cha gari hiyo kuingia na kuzama baharini kimetokana na kile kinachodaiwa kufeli kwa breki wakati dereva wa gari hiyo akikata kona kuelekea upande wa mbele ambapo gari zenye uharaka zinapewa nafasi kukaa mbele pindi kivuko kitakapofika ziwe za kwanza kuingia katika kivuko hicho.

Mashuhuda wanasema gari hilo lilipewa kipaumbele kwani inasemekana lilikuwa limebeba waombolezaji waliokuwa wakienda msibani upande wa Kigamboni.

Taarifa zaidi zinasema wakati dereva wa gari hilo akitafuta namna ya kuegesha (kupaki) gari hilo ndipo gari hiyo ilipofeli breki na kuzama Baharini.

Hadi kufikia hivi sasa juhudi za uokoaji zinaendelea huku baadhi yao wakiwa wameshapoteza maisha.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog