Home » » General News TRA wamekuja na hii ripoti kwa wanaoiba kazi za wasanii

General News TRA wamekuja na hii ripoti kwa wanaoiba kazi za wasanii

Malalamiko ya siku nyingi ya wasanii wa kazi za tasnia ya muziki na filamu kuibiwa au kutumika isivyo kwa kazi zao na wao kutopata chochote kwenye kazi hizo yamesikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA‘ ambapo walianza kulifanyia kazi suala hilo kwa kufanya msako ili kubaini watu wanaoendesha biashara ya kuuza kanda za muziki na filamu bila kufuata utaratibu wa sheria.
April 19 2016 Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA‘ imetoa taarifa kwamba zoezi la msako lilipelekea kukamatwa kwa jumla ya CDs na DVDs 656,579 zenye thamani inayokadiriwa kufikia bilioni 1.3. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa elimu kwa walipakodi , Richard Kayombo amesema ……….
>>>’katika zoezi hilo tulikamata wanaoshiriki kuuza kazi hizi kinyume cha taratibu, tulikamata mitambo 47 ya kudurufu CDs na DVDs pamoja na computer nne ambazo zinatumika katika ufanyaji wa kazi hiyo’:-Richard Kayombo
>>>‘Taarifa za kiinteligesia zinaonyesha kuwa bado kuna CD na DVD nyingi zimefichwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa hiyo zoezi hili ni endelevu na tutawafikia na kuwachukulia hatua za kisheria’:-Richard Kayombo
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog