Home » » Vitu 4 vilivyoongelewa na Mwigulu Nchemba na Ummy Mwalimu baada ya kufika machinjio ya Vingunguti Dar.

Vitu 4 vilivyoongelewa na Mwigulu Nchemba na Ummy Mwalimu baada ya kufika machinjio ya Vingunguti Dar.

April 17 2016 Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba aliongozana na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mpaka kwenye machinjio ya Vingunguti Dar baada ya machinjio hayo kufungiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kwa kutozingatia usalama na usafi wa maeneo ya machinjio.
Baada ya kikao cha muda mfupi kilichofanyika kwenye machinjio  ya Vingunguti Waziri Nchemba aliyaongea haya ‘Kwanza kuna mambo kadhaa tumeyaona ambayo TFDA wamefanya kazi nzuri sana nawapongeza sana wamebaini ukosefu wa maji, na pia visu vinavyotumika kuchinjia vinasafishwa mahali ambapo sio salama vinasafishwa bafuni‘>>>Mwigulu Nchemba Waziri wa  Kilimo Uvuvi na Ufugaji
Sasa tulichokubaliana leo ni kwamba watengeneze baadhi ya sehemu ambazo zinawezekana kwasababu vifaa wanavyo na pili  kati ya leo au kesho waweke zile mashine za kuning’inizia ngo’mbe wakati wa kuchuna , na la tatu warekebishe mabomba ya maji hapa machinjioni‘>>>Waziri wa  Kilimo Uvuvi na Ufugaji Mwigulu Nchemba
Kadri tunavyotaka nyama iwepo katika mabucha yetu wananchi wapate nyama kwa bei nafuu lakini lazima tuhakikishe hiyo nyama ni salama na  imechinjwa katika mazingira safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu, sisi kama wizara ya afya ni wajibu wetu kuhakikisha kanuni za afya na usafi zinazingatiwa’ >>>Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Kwa hiyo nataka kuwatoa hofu watanzania kuwa nyama itakayokuwa kwenye mabucha itakuwa ni nyama salama lakini tutahakikisha tunaendelea kulinda viwango vya nyama ili wasiweze kupata madhara ya kiafya‘>>>Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
3X6A2928
3X6A2933
Sehemu ya mabomba ya maji
3X6A2934
3X6A2937
3X6A2939
3X6A2945Sehemu ya kunin’ginizia ng’ombe wakati wa kuchun
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog