Home » » Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla Aonja Moto wa UKAWA.....Madiwani 34 Wakiongozwa na Meya wao Wasusia Kikao chake cha Kujitambulisha

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla Aonja Moto wa UKAWA.....Madiwani 34 Wakiongozwa na Meya wao Wasusia Kikao chake cha Kujitambulisha

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amekumbana na joto la Mbeya baada ya meya wa jiji hilo, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani wake 34 kususia kikao chake cha kujitambulisha kwa wananchi, baada ya kudaiwa kwenda kukagua Soko la Mwanjelwa bila kumpa taarifa yoyote meya wa jiji hilo.

Meya alifikia uamuzi huo ndani ya ukumbi wa Mkapa muda mfupi kabla ya Makalla kuanza kuzungumza na watumishi wa jiji, wananchi, wazee maarufu, viongozi wa dini na machifu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Sabi alimkaribisha Meya Mwashilindi kuzungumza chochote kwa niaba ya madiwani wake.

Hata hivyo, Meya Mwashilindi alipochukua kipaza sauti alisema: “Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, nakumbuka kwa mara ya kwanza kukutana na wewe tulizungumza kwamba tufanye kazi, siasa zimekwisha. Lakini masikitiko yangu ni kwamba leo hii umekwenda Soko la Mwanjelwa bila ya mimi mwenye jiji kupewa taarifa yoyote wala madiwani wangu. Sasa hiki kikao hakinihusu hivyo muendelee na kikao chenu.”

Baada ya kusema maneno hayo alikabidhi kipaza sauti kwa mkuu wa wilaya, kisha akachukua nyaraka zake akainuka pamoja na madiwani wote kupitia Chadema na kutoka ukumbini huku wakisikika wakisema, ‘hizi ni siasa ambazo tulizikataa, lakini wanatulazimisha kuendesha siasa. Hatuwezi kupuuzwa kwa kiasi hiki.”

Mkuu wa Wilaya, Mnasa alisema anaamini taratibu na ratiba yote ilipangwa vizuri hivyo hawaoni sababu ya madai ya madiwani hao kwamba hawakushirikishwa kwenye ziara hiyo, wao kama wawakilishi wa Rais hawaangalii siasa, bali wanaangalia uchapakazi na siyo masuala ya siasa.

Akizungumzia kitendo cha meya na madiwani wake kususia kikao hicho, Makalla alisema ‘Nashangazwa na uamuzi wa madiwani hawa kwa kitendo hiki, kwani siku ile nilipotembelea Shule ya Sekondari Iyunga, nilisema kwamba Aprili 20 ambayo ndiyo leo (jana) nitakuwa na ziara ya jiji na kabla ya kikao nitataka kutembelea Soko la Mwanjelwa,” alisema Makalla.

Alisema suala la meya na madiwani wake kutoshirikishwa kwenye ziara ya kwenda Soko la Mwanjelwa halimhusu, kwani mwenye wajibu wa kupeana taarifa ni kwenye ngazi ya halmashauri ya jiji, lakini siyo yeye (Makalla).

“Jamani mimi sijaja kufanya siasa nimekuja kufanya kazi ya wananchi na nilishatahadharisha jambo hili, sasa kwa kitendo hiki ndiyo siasa na wananilazimisha kufanya siasa, lakini wao ndiyo watahukumiwa na wananchi. Na ninasema kama Mola ataendelea kunilinda kubaki katika
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog