Home » » Siku alizotoa RC Makonda kwa ombaomba Dar zimetimia, agizo lake je limetekelezwa?

Siku alizotoa RC Makonda kwa ombaomba Dar zimetimia, agizo lake je limetekelezwa?

Siku kadhaa zilizopita Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alitoa maagizo matatu yanayohusu ombaomba wa mabarabarani kuondoka, majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipo kuwa na parking kutafuta parking na wamiliki wa bar kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.
Makonda alitoa muda wa siku sita ambapo muda huo umetimia leo April 18 2016, kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro ameyazungumza haya kuhusu ombaomba mbele ya waandishi wa habari ………
>>>’ombaomba wengi wameanza kuondoka, lakini sisi kama jeshi na idara zingine leo hatukuanza rasmi kwa sababu unapowakamata hawa ndugu zetu lazima ujue namna ya kuwasafirisha na ni operesheni inayohusu idara nyingi, kimsingi vijana wangu wamepita maeneo mbalimbali wameona wengi wameondoka’:-Kamanda Sirro 
>>>’wasije wakafikiria hii ni nguvu ya soda, tunapanga mpango mkakati mzuri kwa wale wachache ambao watakuwa wamebaki’:-Kamanda Sirro
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog