Jeshi
la Polisi linawashikilia vijana zaidi ya 18 wenye umri kati ya miaka 14
na 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya
Wilaya ya Temeke.
Kamanda
wa polisi wa Temeke, Gilles Muroto amesema leo kuwa vijana hao,
wanaohusishwa na kundi la Panya Road linalofanya unyang'anyi maeneo ya
jiji la Dar es Salaam, walikamatwa jana nyakati tofauti baada ya polisi
kuendesha msako wa kuzuia na kupambana na wahalifu.
Alisema
vijana hao wanatoka maeneo ya Buza Kanisani, Chanika, Yombo Kirakala,
Buza Changulu, Yombo Makangawe na moja anayeishi maeneo...
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya April 28 .
Posted by Unknown
Posted on 8:32 AM
with No comments
AINA ZA WASICHANA, TABIA ZAO KIMAUMBILE KATIKA MAPENZI
Posted by Unknown
Posted on 9:01 AM
with No comments

Inasemekana wadada wana tabia tofauti katika mapenzi kulingana na maumbo ya miili yao; karibu Mtembezini uelewe kwa kwa kina vitu vinavyoweza kukusaidia kutambua tabia za watu husika.
1.Wasichana wafupi wanaongoza kwa wivu wa mapenzi na kuwajali wapenzi wao
2. Wasichana warefu huwa hawawajali wapenzi wao na hawaogopi mahusiano kuvunjia hawajui kubembeleza hata kidogo.
3. Wasichana wenye DIMPOZ, MWANYA, MATEGE MBINUKO, MAHIPS NA KITEMBE, hawa huongoza kwa kutokuwa WAAMINIFU katika mapenzi.
4. Wasichana WANENE huongoza kwa kuwa na MAPENZI YA KWELI yaani...
Ripoti ya CAG Yawaweka Kikaangoni Vigogo wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD)
Posted by Unknown
Posted on 8:33 AM
with No comments

Ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad imezichanganya Hospitali ya Taifa Muhimbili na Bohari ya Dawa (MSD), huku Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akihitaji maelezo ya kina kuhusu mkanganyiko huo.
Ummy ameitaka MSD kuandika maelezo ya kina kwa maandishi, kuhusu vifaa vya Sh2 bilioni ambavyo viko njiani kwenda Muhimbili kwa miaka minne sasa, kabla wizara yake haijatoa tamko rasmi.
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu jana alisema bohari haina mzigo wowote ulio njiani kuelekea...
Rais Magufuli Asamehe Wafungwa 3,551
Posted by Unknown
Posted on 7:26 AM
with No comments

Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,551, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja
Jenerali Projest Rwegasira ilisema wafungwa 580 wataachiwa huru, huku
wengine 2,971 watapunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao.
Alisema
rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara
ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliwataja
watakaonufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wenye ugonjwa wa ukimwi,
kifua kikuu na saratani ambao wapo...
Mwenyekiti Aweka Majina HEWA Mradi wa Kuokoa kaya Masikini (TASAF )
Posted by Unknown
Posted on 7:19 AM
with No comments

Wananchi
wamemkataa mwenyekiti wa kitongoji cha Mwanogi kijiji cha Bulima, Kata
ya Nyashimo wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu, wakimtuhumu kuweka
majina hewa katika mradi wa kuokoa kaya masikini unaosimamiwa na Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
Mwenyekiti huyo wa kitongoji, Ester Ng’ombe anatuhumiwa pia kufanya kazi kwa ubaguzi wa vyama vya siasa.
Akizungumza
katika kikao, mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha
Bulima, Zablon Ntinika alisema wamefikia uamuzi wa kumsimamisha kazi
mwenyekiti huyo baada ya uchunguzi walioufanya kubaini majina matano
ambayo...
Mwanafunzi Amkaanga kortini polisi anayedaiwa kumbaka katika kibanda cha ulinzi cha benki.
Posted by Unknown
Posted on 7:02 AM
with No comments

Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga
askari polisi anayedaiwa kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi
alivyotendewa kitendo hicho katika kibanda cha ulinzi cha benki.
Akitoa
ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Misungwi, Ruth Mkisi,
shahidi huyo alidai siku ya tukio askari huyo, Raphael Sixstus (30),
alimuita alipokuwa akipita karibu na Benki ya CRDB Tawi la Misungwi,
alipoitikia wito ghafla alivutiwa ndani ya kibanda hicho na kumbaka.
“Wakati
akinitendea kitendo hicho, alikuwa akinitishia kisu huku akiniambia
nikipiga kelele ataniua, niliogopa nikaa kimya ingawa...
Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 27 2016 kwenye, Udaku, Hardnews na michezo
Posted by Unknown
Posted on 6:58 AM
with No comments
AGIZO LA MAKONDA ,Polisi Dar Yakamata Ombaomba 45 Dar, 17 Wapelekwa gerezani
Posted by Unknown
Posted on 9:23 AM
with No comments

Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa
jeshi hilo kwa kushirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii, wanafanya
utaratibu wa kuhakikisha watu hao wanarudishwa mikoani walikotoka.
“Kazi
hii inaenda vizuri na ombaomba wachache wamebakia ambao wakiwaona
askari wanakimbia na kutokomea kusikojulikana,”alisema Sirro.
Katika
tukio lingine, Polisi wanawashikilia watuhumiwa 96 wenye umri wa miaka
15-18 wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya kuvamia nyumba na kuiba
usiku.
Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao wanajulikana...
Mchina Ahukumiwa Miaka Mitatu Jela Kwa Kuuza Bidhaa Bila Kutoa Risiti
Posted by Unknown
Posted on 9:11 AM
with No comments

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au
kulipa faini ya Sh4.5 milioni, mfanyabiashara Huifang Ma baada ya
kupatikana na hatia ya kuuza bidhaa na kushindwa kutoa risiti kwa
kutumia mashine ya kieletroniki.
Ma ambaye ni raia wa China na mkazi
wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la Kariakoo, alihukumiwa kifungo hicho
baada ya kukiri mashtaka mawili yaliyokuwa yakimkabili likiwamo la
kushindwa kujisajili kulipa kodi ya ongezeko la thamani (Vat).
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said
Mkasiwa...
Wafanyakazi wa TMA watakiwa kutumia mfumo wa kisasa kuhifadhi taarifa muhimu za ofisi
Posted by Unknown
Posted on 9:05 AM
with No comments

Watumishi
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, (TMA) wametakiwa kuachana na mfumo
wa zamani wa kutumia makaratasi katika kuhifadhi taarifa zao muhimu na
badala yake kuanza kutumia mfumo wa kisasa wa kieletroniki.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Pof. Makame Mbarawa jana
jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wafanyakazi hao na kueleza
kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza matumizi ya fedha za
kununulia karatasi.
“Katika
ofisi zenu nimeona kila mtu anakomputa ni jambo zuri hivyo zitumieni
katika kuhifadhi taarifa muhimu...
Ripoti ya CAG Yaanika 'Madudu' Kibao Serikalini
Posted by Unknown
Posted on 7:26 AM
with No comments

Wakati Rais John Magufuli akipambana dhidi ya ufisadi, uzembe na
ukwepaji kodi na uovu mwingine dhidi ya mali za umma, ripoti mpya ya
ukaguzi iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
inaonyesha ana kazi kubwa zaidi kupata ushindi kwenye vita hiyo.
Ripoti
hiyo ya mwaka 2014/ 2015 iliyowasilishwa bungeni jana na CAG Mussa Juma
Assad imeibua uozo zaidi kwenye halmashauri, taasisi za Serikali na
mashirika ya umma, ikibainisha kuwa nchi ina tatizo kubwa zaidi ya watu
ambao wamekuwa wakishughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Ripoti
hiyo...
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 26 .
Posted by Unknown
Posted on 7:07 AM
with No comments