Home » » Waliopitishwa kuwania uspika CCM, masharti kwa mgombea unaibu je?

Waliopitishwa kuwania uspika CCM, masharti kwa mgombea unaibu je?


Nape Nnauyecomments
Katibu mkuu wa itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye akizungumza na wana habari.
Kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ilikuwa na kikao cha siku moja  kilichofanyika leo Novemba 15, 2015 mjini Dodoma na imewateua wana-CCM watatu ambao watakaopigiwa kura na wabunge wote wa CCM ili kumpata mgombea wa CCM katika nafasi ya spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa kugombea nafasi hiyo na kamati kuu iliyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni pamoja na naibu spika aliyemaliza muda wake Job Ndugai, Dkt. Tuliana  Ackson na Abdullah Mwinyi.
Job Ndugai
    Job Ndugai
Dkt. Tuliana Ackson
 Dkt. Tuliana Ackson
Abdulah Mwinyi
 Abdullah Mwinyi
Wana-CCM hao watatu watapigiwa kura wakati wa kikao cha kamati ya wabunge wote wa CCM kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za makao makuu ya CCM Dodoma ili kuchagua jina moja kugombea nafasi hiyo katika bunge la jamhuri ya muungano.
Katibu mkuu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameyazungumza haya>>
Ibara ya 57, Kanuni za kamati ya wabunge wote wa CCM toleo la 2010 toleo la nne 2011, mbunge yeyote anayetaka kugombea nafasi ya naibu spika atatakiwa kuchukua fomu kupitia kamati hiyo na atairudisha kisha kamati itakaa kupata jina moja,”
Kwa mujibu wa maelezo hayo mbunge wa chama hicho anayetaka kugombea unaibu spika, atatakiwa kuchukua fomu leo Novemba 15, kwa ada ya Sh 100,000 kisha atairudisha kesho Novemba 16, ndipo kamati itakaa kuchambua na kupitisha jina moja” ,- Nape Nnauye
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog