Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo usiku wa November 9 alifanya uzinduzi rasmi wa movie yake ambayo anataja kuiandaa kwa ajili ya mashabiki wake, Ronaldo kafanya uzinduzi movie yake inayoitwa ‘Ronaldo’ akiwa pamoja na mama yake na mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior.
Uzinduzi huo uliyofanywa Leicester Square katika jiji la London Uingereza ulihudhuriwa na makocha wa zamani wa staa huyo ambao ni Sir Alex Ferguson, Jose Mourinho na Carlo Ancelotti sambamba na uwepo wa wakala wake Jorges Mendes na mastaa wengine wengi.

Ronaldo akiwa na kocha wake wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson aliyekuwepo katika uzinduzi huo.
Movie hiyo ambayo imechezwa kwa zaidi ya
miezi 14 kwa asilimia kubwa inahusisha maisha halisi ya staa huyo
ambaye alianzia maisha yake soka katika klabu ya Sporting Lisbon ya kwa Ureno, Ronaldo amefanya uzinduzi huo sambamba na kufanya interview fupi katika red carpet.
Hii ni sehemu ya interview ya Ronaldo katika uzinduzi huo



0 comments:
Post a Comment