HII NI HATARI HATA KAMA NI UMASIKINI????????? DUH!!!!BINTI ALIYEONGOZA MATOKEO YA DARASA LA SABA AOZESHWA KWA MAHARI YA KILO 2 ZA SUKARI.
Pamoja
na Serikali kuendelea kupiga vita wazazi kuwaoza mabinti zao wakiwa bado wadogo
lakini bado kuna baadhi ya makabila hapa nchini wameendeleza utamaduni huo kwa
kuwaoza mabinti zao sababu kubwa ikitajwa kuwa ni tamaa za kutaka
kujilimbikizia mali.
Lakini kwa msichana huyu wazazi wake wameonekana kutoijali hata
ile mali waliyopewa kwani wameweza kumwozesha binti yao wa kike kwa mahari ya
kilo mbili za sukari toka kwa mfugaji wa kabila la kimasai.
Gazeti la NIPASHE limeripoti kuwa mmoja wa wanafunzi walioongoza
darasa wa Taifa wa Darasa la saba mwaka huu mwenye umri wa miaka 16 anadaiwa
kuozwa kwa mwanaume mwenye miaka 50 baada ya wazazi wake kupewa sukari kilo
mbili kama mahari.Kutokana na hali hiyo mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu
ukeketeji Mkoani Kilimanjaro NAFGEM umefanya jitihada za kumuokoa pamoja na
wanafunzi wengine15 waliotaka kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa ngariba.
Msichana huyo wa miaka 16 wa kabila la kimasai ambaye jina lake
limehifadhiwa baada ya kufaulu mtihani huo kwa asilimia kubwa huku akitajwa
kuwa miongoni mwa wasichana waliofanya vizuri aliozeshwa kwa mwanaume mmoja
ambaye ni mfugaji wa kabila hilo.
Meneja Mpango wa mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketaji
Mkoani Kilimanjaro Honoratha Nasua alitoa taarifa za kuolewa kwa binti huyo
walizipatahuku wanafunzi wengine 15 wakisubiri tarehe ya kufanyiwa ukeketaji
ili waozeshwe baada ya tendo hilo.
Alisema suala la mwanafunzi huyo aliyeozeshwa limefikishwa katika
dawati la jinsia la Polisi Wilayani Siha kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za
kisheria.
Alisema wazazi wa mwanafunzi huyo wamechangia kudidimiza maendeleo
ya mtoto wao kwa kukubali aolewe na kubuni mbinu mpya ya kukeketa watoto
wachanga ili kukwepa mkono wa dola na vyombo vya wanaharakati.
Mtandao huo wa kupinga ukeketaji unaendelea na shughuli zake
katika Wilaya hiyo ikishirikiana na Shirika la kimataifa la Elimu kwa ufadhili
wa Shirika la misaada la kimataifa la Marekani USAID kupitia mpango wa pamoja
wa TUWALEE!
0 comments:
Post a Comment