Home » »

Watu wawili walivyochomwa moto Buguruni baada ya kuhusishwa na wizi wa bodaboda.

Kumekuwa na ripoti za wizi wa bodaboda kutoka sehemu mbalimbali, tukio limegusa kwenye Hekaheka ya ‘Leo Tena‘ inatokea Buguruni… madereva wa bodaboda wamewakamata watu wawili, mwanamke na mwanaume wakidai wanahusika na wizi wa bodaboda.
Kilichofanywa na watu hao wa bodaboda walimkamata kwanza jamaa huyo, akapelekwa eneo la Buguruni Sukita, wakampiga na kumchoma moto… mpaka Polisi wanafika tayari mwili wa jamaa huyo ulikuwa umeteketea wote kwa moto.
Muda mfupi baadae vijana hao walirudi na mwanamke waliyedai amekuwa akishirikiana na jamaa huyo kwenye wizi, na yeye walimpiga na kumfanyia vitendo vya kikatili… Watu wa jirani na eneo hilo wamesema jitihada za kuwaokoa watu hao hazikufanikiwa kwa sababu vijana wa bodaboda walikuwa wengi wakawazidi nguvu…
Polisi waliwahi kufika na kumuokoa japo ana majeraha makubwa sana, kwa sasa anapatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog