Naibu
Gavana wa Jimbo la Shandong , Xia Geng( kushoto)akionesha moja ya
tisheti zinazotengenezwa nchini kutipia mwekezaji kutoka nchi hiyo
kwenye Mamlaka ya Ukanda Maalum waUwekezaji Tanzania (EPZA) leo mara baada ya kutembelea eneo hilo jijini Dares Salaam.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda kesho anatarajiwa kuwa mgenio rasmi katika mkutano
wa majadiliano wa ushirikiano wa Serikali za Mitaa za China na Tanzania
utakaofanyia katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.
Nyerere jijini Dares Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ilitotolewa na Ofisi ya Waziri
Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI imeeleza kwamba
mkutno huo ni miongoni mwa mambo yatakayofanywa katika ziara ya wajumbe
wa watu wapatao 70 kutoka Serikali za Mitaa kutoka China, wakiwemo
magavana,mameya na wafanyabiashara ambao wamewasilini nchini tangu jana
ikiwa ni mikakati ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa
za Tanzania na China.
“
Ujio wa wageni hawa unafungua ukurasa mpya wa urafiki na kusaidia
kuleta maendeleo na utoaji wa huduma nzuri kwa jamii na kiuchumi,”
ilisema taarifa hiyo.
Ujumbe huo pia utakutana na baadhi ya Mawaziri wa Sekta mbalimbali, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa.
Wengine
watakaokutana nao ni baadhi ya Mameya/Wenyeviti wa Halmashauri za Jiji,
Manispaa, Miji na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri,Taasisi
za Serikali na Binafsi pamoja na Wafanyabiashara.
Wakati
huohuo Serikali ya China imesema iko tayari kushirikiana na Tanzania
kuboresha miundombinu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
ili kuweza kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Makamu wa Rais wa Umoja wa Wachina wenye
Urafiki na nchi za Nje, Feng Zuoku mara baada ya ujumbe huo kutembelea
, reli hiyo , Makumbusho ya Taifa na Mamlaka ya Ukanda Maalum waUwekezaji Tanzania (EPZA) jijini Dares Salaam.
Tumejifunza
mengi katika ziara hii.Tutaendelea kuimarisha ushirikiano katika
masuala ya miundombinu, biashara na uchumi,” alisema Rais huyo.
Aliongeza kuwa waomeona miundombinu ya EPZ ni mizuri hivyo wawakezaji kutoka nchi hiyo wako tayari kuja kuwekeza.
Akizungumzia kuhusu Makubusho ya Taifa alisema wamejinza mambo mengi ya historia ya Tanzania ambayo inafanana na China.
Rais
huyo aliwapongeza Watazania kwa ukarimu wanaouonesha kwao , hivyo
wanategemea baada ya ziara hivyo ushirikino huo utaingia katika sura
mpya.
|
0 comments:
Post a Comment