Home » »

BINTI ATISHIWA KUCHINJWA NA KUSILIMISHWA KWA NGUVU NIGERIA

Hajja ©Reuters/Joe Brock
"Nilipolia walinipiga, na nilijaribu kuongea pia walinipiga. Waliniambi aninlazima nisilimu kuwa Muislamu ili wasiniue". Hajja anasimulia, binti mwenye umri wa miaka 19, ambaye amepona kwenye mikono ya kundi la kigaidi lenye uhusiano na al-Qaeda, Boko Haram nchini Nigeria.
Milima ya Gwoza ndiko ambako kijiji cha binti Hajja kinapatikana, ambapo kuna siku alikuwa kwenye shughuli za kawaida alipotekwa na kundi hilo, na kulazimishwa kuzunguka nalo kwa miezi mitatu huku akiwapikia na kuwafulia nguo zao.
Katika ushuhuda ambao ameueleza kwa shirika la habari la Reuters, Hajjaa anasema kuwa. licha ya kwamba hakubakwa, ila alikuwa akiteswa vibaya sana na kulazimishwa kuachana na Ukristo, ili apate kuishi, jambo ambalo alikuwa akipingana nao kwa nguvu, hatua ambayo ilimfanya mmojawapo wa watekaji kumbembeleza ili asiuawe kwa kuchinjwa, ambapo siku moja kabla tu hajauwawa ilimbidi akubaliane nao na kuapishwa - na kisha kulazimishwa kusoma Quran.
Kati ya mayeso ambayo ameyapata, Hajja anaeleza kuwa alikuwa ni mtu wa kufua na kupika, na kama hakuwa akifanya hizo shughuli basi alilazimishwa kubeba silaha zao, na kisha siku moja hatosahau ni pale ambapo walimfanya chambo/mateka mbele ya wanajeshi wa serikali ili wasidhurike wala kukamatwa.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog