Home » »

ANGALIA PICHA ZA SHANGILIENI KWAYA WAKIWA AFRIKA YA KUSINI KIHUDUMA

Kwaya ya Tumaini Shangilieni toka St.James Kaloleni Arusha inatarajiwa kuwasili siku ya leo ikitokea nchini Afrika ya kusini ambako ilikwenda katika kanisa la Anglican kitongoji cha Tembisa jijini Johannesburg kihuduma. Kwaya hiyo ambayo iliondoka na ndege ya Fastjet siku ya ijumaa, imefanikiwa kufikia lengo lililowapeleka nchini Afrika ya kusini kumuhubiri Kristo.

Wakati huohuo taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba kwaya hii inatarajiwa kuwepo usharika wa Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam siku ya tarehe 8 mwezi ujao katika kuwasindikiza kwaya ya uinjilisti Kijitonyama ambayo itakuwa ikisherehekea miaka 25 ya kwaya yao tangu ilipoanzishwa.


Taarifa kamili na picha nyingine zitawajia kupitia hapa hapa GK. Kwa leo pata japo kwa kifupi
Mawinguni mwe!
Muonekano wa jiji la Johannesburg kutokea juu karibu na uwanja wa ndege wa OR Tambo.
Mwenyekiti wa Tumaini Dkt. Emanuel Mtangoo na wanakwaya wengine wakizungumza na mwenyeji wao mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa OR Tambo.
Safari ya kuelekea kanisani.
Usharikani Tembisa.
Waimbaji wa Tumaini wakiwa kanisani siku ya jumapili.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog