Home » »

AFLEWO YAKUTANISHA WACHUNGAJI KUELEKEA TAMASHA LA 2014

Wachungaji katika picha ya pamoja baada ya majadiliano
Kukutana huko kumetokea siku ya Jumanne katika Hoteli ya Peacock Dar es salaam, ambapo kumeambatana na chai ya asubuhi (Pastor’s Breakfast) kwa lengo la kuwashirikisha wachungaji hao maono na mipango ya huduma ya Afrika Let's Worship AFLEWO 2014 na pia kuomba ushiriki wao na wa washirika wao katika maandalizi kwa ajili ya mkesha huo wa kusifuna kuabudu unaotegemea kufanyika mwakani mwezi wa sita.

Kusanyiko limetokea siku chache kabla ya uzinduzi wa usajili na Mass Kwaya ambapo unaanza Jumapili hii saa 9:00 mchana Katika kanisa la City Christian Centre (CCC) Upanga jirani na Chuo cha mzumbe, usahili huo utaendelea mpaka Januari na kufunga usajili wa kujiunga na Mass Kwaya hiyo,

Jumanne hiyo, kusanyiko hilo lilikuwa likiongozwa na Walezi wa huduma ya AFLEWO Tanzania  ambao ni Pastor Paul Safari (DPC), Bishop Fredrick Kyara (P.C.E.A St. Columbus), Mwenyekiti Geoffrey Obielo na Administrator wa AFLEWO Tanzania Anna Abella Munyagi.
Baadhi ya mambo yaliyozungumzwa ni pamoja wao na kuwa walezi wa AFLEWO wa sehemu kidogo katika kutoa ushirikiano pale itakapotakiwa,huduma zao kusaidia kuwa ruhusu waumini wenyewe uwezo wa kuimba kuja siku ya Jumapili kujiunga na AFLEWO Mass Kwaya, tutakapo karibia siku ya tukio mwakani kutoa nafasi yaAFLEWO kwaya kuhudumu Makanisani kwao ikiwa ni sehemu kuitangaza na taarifa kuwafikiwa watu katika makanisa mbalimbali ili wahudhurie mkesha huo.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog