JAMAA AMUUA MKE WAKE KWA KUMCHINJA NA KISHA KUMTOBOA KIFUANI WAKIWA GESTI HUKO DAR

Mwili wa marehemu

Mtuhumiwa wa mauaji
Mkazi
wa Tabata Mawenzi, Remi Joseph (36) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma
za kumuua mkewe kwa kumkata kichwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends
Corner ya jijini Dar es Salaam.
Aliyeuawa
ni Josephena Moshi (35), ambaye alikatwa kichwa na kuchomwa na kitu
chenye ncha kali kifuani wakiwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends
Corner.
Akihojiwa
kuhusiana na tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa
Kinondoni, Augustine Senga, alikiri kutokea mauaji hayo.
Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi saa 8:00 mchana na kwamba familia hiyo ilikuwa inaishi Tabata Mawenzi.
Senga
alisema mwanamke huyo alifariki papo hapo baada ya kushambuliwa na
kwamba chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.
Kamanda
Senga alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
ya Muhimbili na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.
Hata
hivyo, gazeti hili lilijulishwa kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kufanya
mauaji hayo, alifanya jaribio la kutaka kujiua lililoshindikana.
Kamanda alipoulizwa kuhusiana na mtuhumiwa huyo kutaka kujiua, alisema kuwa uchunguzi unaendelea.
“Bado
ni mapema sana kueleza kila kitu hayo niliyokueleza ni taarifa za awali
kwani na huyu mtuhumiwa amekutwa na majeraha shingoni, hivyo masuala ya
kazi yake na sababu vinachunguzwa,” alisema Senga.
Na Beatrice Shayo-Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment