BABA AKUTWA AMEKUFA KWENYE BWAWA LA MAJI HUO SHINYANGA, MKE ADAI ALITOKA USIKU KUJISAIDIA
.
Mwili wa Marehemu Charles Makima ukitolewa kwenye Maji hayo
Mkazi
wa kitongoji cha Nyashimba kijiji cha Solwa, Wilayani Shinyanga
Vijijini Mkoani Shinyanga, Charles Makima (50-55) amekutwa amekufa maji
katika bwawa la Sululuni lililopo katika kijiji hicho.
Mashuhuda
wamesema Marehemu Makima amekutwa akielea juu ya maji katika Bwawa hilo
jana majira ya saa kumi na moja jioni na ndipo taarifa ilipotolewa kwa
wananchi na uongozi wa kijiji kwa ajili ya kuutoa mwili huo ndani ya
maji.
Wananchi wa Kijiji cha Solwa Wakiutazama mwili wa Marehemu Charles Makima
Kwamujibu
wa mke wa Marehemu ambaye jina lake halijapatikana mara moja, amesema
mumewe alitoka usiku wa kuamkia jana kwenda nje kujisaidia lakini
hakurudi tena, na walifanya jitihada za kumtafuta bila mafanikio hadi
alipokutwa katika bwawa hilo.
Chanzo
cha tukio hilo bado hakijafahamika lakini imedaiwa kuwa Marehemu Makima
alishawahi kufanya jaribio la kujiua kwa kujikata kisu shingoni mnamo
mwaka 1984.
Hata
hivyo baada ya Mwili huo kuopelewa na wananchi, umepelekwa nyumbani kwa
Marehemu kuhifandhiwa hadi hapo jeshi la polisi litakapofika kwa ajili
ya uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment