"Mtu yeyote anayeiombea amani anaipenda nchi hii. Leo natoa changamoto waimbaji wa nyimbo za injili wahubiri sana amani."
Ni kauli ya Waziri Mkuu aliyepita, ambaye pia ni mbunge wa Monduli, Mh.
Edward Lowassa, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa DVD ya
album ya Dunia Haina Huruma, ya kwake Bahati Bukuku, ambayo imehudhuriwa
na maelfu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa PTA,
viwanja vya Sabasaba Jumapili hii.
Gospel Kitaa ilikuwepo kna kushuhudia ambapo, pamoja na kuwataka
waimbaji wa nyimbo za injili wahubiri amani, Mh. Lowassa pamoja na
marafiki zake walichangia kiasi cha shilingi Milioni 20.
Waimbaji kadhaa walimsindikiza Bahati kwenye uzinduzi huo ambao haukuwa
na kiingilio, ambapo injili ilihubiriwa kwa njia ya uimbaji na watu
kukata kiu na njaa ya kiroho waliyokuwa nayo, mkongwe Jennifer Mgendi,
Bonny Mwaitege, Neema Gasper, Rebecca Magaba (Ebenezer), Emmanuel Mgogo
(Msikilize Mungu), Majestic Singers wa EAGT Singers, Sarah Mvungi, ni
sehemu tu ya waimbaji waliokuwepo.
Jennifer Mgendi akihudumu |
MC wa shughuli, Silas Mbise akishuhudia mgeni rasmi anavyopungiwa |
Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akiwaaga wananchi |
0 comments:
Post a Comment