NIWAKATI WA KUOMBA DUNIA SASA IMEHARIBIKA

HIVI NDIVYO MWANANCHI WA KIJIJI CHA WENDA ALIVYOCHUNWA NGOZI


Hivi ndivyo  mkazi  wa Wenda  alivyochunwa  ngozi na  watu  wasiojulikana (Tunaomba Radhi kwa  picha hizi )

Hii  ndio  nyumba  ulimokutwa mwili  wa  mkazi huyo

eneo la  tukio



Baada ya siku mbili mtandao huu kuripoti tukio la kusikitisha kilichohusisha mauaji ya kinyama ya dereva wa bodaboda sadiki mbelwa (26) katika kijiji cha wenda, Tanangozi Iringa ambapo mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na majeraha sehemu za kichwani huku ikisadikiwa kupigwa na kitu chenye ncha kali.
eo katika tukio lingine la kusikitisha ambalo limetokea katika kijiji cha wenda kitongoji cha Lupeta amekutwa mwili mwanakijiji aliyetambulika kwa jina la Leornad Kutika (49.

Mwili wa marehemu kutika umekutwa katika nyumba aliyokuwa akiishi huku ukiwa umechunwa ngozi, kunyofolewa macho pamoja na kukatwa sehemu za siri.

Akingea na mtandao huu wa huzuni baba mdogo wa marehemu Martin Kutika mkazi wa lupeta anaeleza kuwa usiku wa kuamkia jana alipigiwa simu ndugu wa marehemu aliyefahamika kwa jina Kibadeni kutika kuwa ndugu yake huyo ambayekwa mujibu wa maeezo yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la akili alikutwa katika nyumba aliyokuwa anaishi huku akiwa amefariki na kuondolewa sehemu za siri na kuchunwa ngozi. Zwadi mwenga ambaye pia ni ndugu wa marehemu anaeleza kuwa alipata taarifa za tukio hilo jana na ndipo alipofika katika nyumba ya marehemu na kukuta akiwa amefariki.

Akilelezea kuhusu tatizo alilokuwa nalo marehemu Mwenga amesema marehemu alianza kusumbuliwa na tatizo la kurukwa akili tangu alipokuwa mdogo japo hakuwahi kufanya vurugu yoyote na wao kama familia wamekuwa wakimpatia chakula na siku mbili kabla ya tukio marehemu alionekana lakini baada ya hapo hawakumuona tenda ndipo wifi yake alipofika nakukuta marehemu amekufa huku akiwa ametendewa unyama huo.
 Afisa mtendaji wa kijiji cha wenda Dismas Ngweta anaeleza kuwa alipigiwa simu na mwenyekiti wa kjjij cha lupeta Geofrey Dugange nakumweleza kuwa hakuna amani katika kijiji hicho kuwa kuna mwanankijiji ambaye ameuawa. Akielezea baada ya kufika eneo la tukio Ngweta anaeleza kuwa walipouangalia mwili wa marehemu waligundua kuwa amechunwa ngozi, kunyofolewa macho, kukatwa sehemu za siri pamoja na kutobolewa katika sehemu ya mguu. Akilinganisha tukio hili na lililotokea siku chache zilizopita Ngweta ameeleza kuwa tukio la dereva wa bodaboda limetokea wakati wa usiku na kusema kuwa inasemekana kuwa tukio la pili limetendeka usiku kwani kwa mujibu wa wanakiji walieleza kumwona marehemu jioni kabla ya tukio.

 Je nijuhudi gani zimefanywa na jeshi la polisi mpaka sasa? Ngweta ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hilo alipiga simu kwa mkuu wa kituo cha ifunda naye akajibu kuwa awasiliana na wa kituo kikubwa Iringa. Mpaka mtandao huu unatoka eneo la tukio hakuna afisa usalama aliyekuwa amefika katika eneo hilo.

Tukio hili ni la mara ya pili kutokea baada ya tarehe 25 Septemba kuripotiwa kuuwawa kinyama kwa dereva wa bodaboda na pikipiki yake kutoonekana.

MADAM RUTI ALIA NA MAKANISA



Mwimbaji wa muziki wa injili nchini, Madamu Ruti Mwamfupe amedai kulizwa na makanisa yanayoshindwa kuwasaidia watu wenye uhitaji kama wagonjwa waliolazwa hospitalini.

Akizungumza  Dar es salaam jana, Madamu Ruti alisema hospitalini kuna baadhi ya watu ambao hawana fedha za kununua hata chakula, wakati watumishi wa Mungu wanakula na kusaza.''
Hata vitabu vitakatifu vinasema; dini iliyosafi isiyo taka mbele za Mungu Baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao ya kujilinda na dunia,'' alisema Madamu.

Mwimbaji huyo alisema, endapo makanisa hayo yangejiwekea utaratibu wa kuwasaidia wagonjwa kila wiki, ingewawezesha baadhi yao kupona haraka. Alisema wagonjwa wengi wanachelewa kupata uponyaji kutokana na kushindwa kupata mlo bora, licha ya kutumia dawa zinazohitaji kula chakula kingi.

Mwimbaji huyo hivi karibuni alikwenda kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road na kutoa misaada ya vitu mbalimbali, vyenye thamani ya sh. 700,000 na fedha taslimu sh. 500,000.

ASKOFU MWASOTA AVUNJA UKIMYA TUHUMA ZA KUNASWA NA KUNDI LA FREEMASON

Askofu David Mwasota, katibu wa baraza la makanisa ya kipentekoste nchini CPCT.
                         
Hatimaye Katibu Mkuu wa Baraza la makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) Askofu David Mwasota, amevunja ukimya wa tuhuma zilizosambazwa sehemu mbali mbali zikieleza kuwa amenaswa na kundi la siri la waabudu shetani Freemasons.

Akiongea na chanzo cha habari cha blogger kwa uchungu, Askofu Mwasota alisema:

“Ndugu yangu naona haya ni mashambulizi, nimezushiwa mengi achilia mbali yaliyoandikwa na magazeti, jumbe zinasambazwa kwa watumishi wa Mungu (wachungaji) wakae mbali na mimi eti nimekuwa freemason, lakini haya yote ni mashambulizi tu…”

Akifafanua zaidi alisema: “Nakwambia ukweli kutoka moyoni mwangu, sijui hata kiongozi mmoja wa kundi la Freemasons, wala sijui hata hekalu lao liko wapi, mimi nilikuwa nafundisha kanisani nikawaonya wapentekoste wakae mbali na watu wasiowajua kwa kuwa wengine ni waabudu shetani, na wanawajia kama watu wema ili kuwarubuni,”alisema kiongozi huyo na kuongeza:

“Nikatoa mfano wa waumini wangu na mimi mwenyewe, nakumbuka niliwaambia kuwa niliwahi kuhudhuria semina moja na baada ya kukamilika nilipewa nishani ambayo  baadaye nilikuja kubaini kuwa ilikuwa na nembo nisisozielewa, sikusema ni nembo za Freemasons, nilisema  nisizozielewa, nikaamua kuitupa hiyo nishani, lakini naona waandishi waliamua kunimaliza, namwachia Mungu aamue kati yetu…”

Alipoulizwa ni semina gani hiyo na kama anauhakika kuwa nembo alizoshtukia sio za kundi hilo, alijibu:

“Sikia ndugu…nilichosema kilikuwa ni mfano tu wakati nahubiri, nilimaanisha kuwa nembo hizo sikuwa na uhakika nazo, hiyo haimaanishi zilikuwa ni za kundi la Freemasons, nimekwisha kueleza sijui hata kiongozi mmoja wa kundi la Freemasons,  wala sina haja nao, mimi nimeokoka naenda mbinguni waabudu shetani ni wanini?”

“Jambo la kustaajabisha zaidi ni kuwa wewe ndio Mwandishi wa kwanza kuongea nami, kuhusu jambo hili kwa mapana yake, wengine walinipigia simu nikawaambia waje ofisini sikuwaona, lakini nikashtukia habari kubwa imeandikwa, hii inaniuma sana…”

Askofu Mwasota, alisema kuwa ameshauriwa juu ya jambo la kufanya na anajiandaa kuchukua hatua kwa kuwa anaona kuwa kuna njama mbaya dhidi yake, huduma anayoiongoza na kanisa la Mungu kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa katika ibada hiyo lengo la mahubiri yake lilikuwa ni kuwaonesha wapentekoste hatari iliyopo mbele yao kwa kuwa makundi hayo ya waabudu shetani yapo na yanawawinda.

“Mimi ni Askofu na kiongozi wa baraza la Wapentekoste, ilikuwa ni wajibu wangu kuonya wenzangu, lakini mifano yangu ilipinduliwa kwa makusudi. Nadhani wakati nahubiri kulikuwa na mwandishi wa (jina linahifadhiwa) ambaye aliichukua kama alivyotaka,” alisema Askofu Mwasota.

Kwa karibu wiki nzima kumekuwa na jumbe mbali mbali zinazosambazwa kupitia simu zikieleza kuwa Askofu Mwasota amenaswa na kundi la Freemasons na kuwataka wapentekoste kukaa mbali naye.

Baadhi pia ya waumini wa makanisa ya Kipentekoste na hata wachungaji wamekuwa wakiulizana huku na kule wakitaka ukweli kuhusu habari za kiongozi huyo wa ngazi ya juu katika baraza la Wapentekoste kutajwa na kundi hilo.

Kutokana na kiu hiyo ya watu wa Mungu, Blog hii  liliamua kuchunguza ukweli wa jambo hilo kuanzia kwa Askofu mhusika na vyanzo vingine vya habari ili kutoa jibu kwa wenye kuguswa na mkanganyiko huo.

Baadhi ya watu wa karibu na Askofu Mwasota, waliofanya mahojiano ya siri nachanzo kimoja cha blog wameeleza wasi wasi wao kuwa kuenea kwa kasi kwa habari hiyo na mazingira yake vinaashiria kuwa huenda kuna mbegu ya chuki inayochochea jambo hilo.

Mmoja wa watu waliohudhuria ibada siku Askofu Mwasota alipohubiri na kuwaonya watu kukimbia makundi ya wale wanaowajia ghafla kama malaika wa nuru, alisema:

“Mimi nilikuwa kwenye ibada siku Askofu Mwasota alipohubiri na kutoa mifano; nilichosikia akisema ni kuwa alihudhuria semina na mwisho akapewa nishani ambayo baadaye alibaini kuwa na nembo, ambazo hakuwa na  uhakika nazo na kwa kutotaka kujichanganya akaamua kuitupa, wala hakusema kuwa amehudhuria mkutano wa Freemasons.”

Katika siku za karibuni kumekuwa na mlipuko wa makundi ya vijana wanaosaka jinsi ya kujiunga na kundi la Freemasons wakidai eti ni suluhisho la maisha magumu.

Habari za kuenea kwa kasi kwa kundi la Freemasons zimekuwa zikivuta hizia za watu wengi, wengine wakidhani kuwa kujiunga nao kunaweza kuwafanya kuwa tajiri.

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO


Mtuhumiwa alijifunika kwa kofia akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi
Gari lililomleta mtuhumiwa
Siku ambayo Daudi Mwangosi alipouwawa kwa bomu katika kijiji cha Nyololo Mufindi
Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa mahakamani.

mwandishi maalum wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Iringa anaripoti kuwa ,Mtuhumiwa huyo amefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu Michael Luena, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.

Amesema mtuhumiwa huyo mnamo Septemba 02mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.


Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambalo limewaletea ugumu waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe picha.

Kila wakati waandishi walipotaka kupika picha walikuwa wakisukumwa na askari hao huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuziba uso kuhakikisha kuwa sura yake haionekanai na waandishi hao.

Katika hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa gari binafsi la kifahari lenye namba za usajili T 320 ARC Toyota Land cruiser GX tofauti na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi.

MASHABIKI WA PASTOR BENJAMIN DUBE WAACHWA NA SIMANZI NCHINI SWAZILAND

Pastor Benjamin Dube akimsifu Mungu katika moja ya recording zake.
                             
Mashabiki wa mwimbaji nguli wa muziki wa gospel pastor Benjamin Dube nchini Swaziland wamefikwa na huzuni baada ya onyesho lililokuwa limepangwa kufanyika katika uwanja wa trade fair hii leo kuahirishwa kutokana na wahusika waliotaka kumkaribisha mwimbaji huyo kushindwa kutimiza mahitaji hali iliyomfanya mwimbaji huyo kuwaomba radhi mashabiki wake na kuwataka kumsubiri hadi tarehe 10 mwezi November mwaka huu atakapokuwa na ziara nchini humo.

Licha ya ziara ya mwimbaji huyo ktokuwepo wikiendi hii huko Swaziland lakini taarifa alizozipata kutoka kwa mashabiki ni kwamba matangazo ya runinga kuhusiana na onyesho lake bado yanatangazwa jambo ambalo limemsononesha.

Mwimbaji huyo katika ratiba yake mwisho wa wiki hii  atakuwa katika mji wa Klerksdorp, Botswana na hapo kesho alitarajiwa kuhitimisha ziara yake huko Swaziland lakini sasa haitawezakana ambapo tayari amewaomba radhi mashabiki wake waliokuwa wakimsubiri kwa hamu.Lakini pia hakuacha kuwaambia wapenzi wake kuwa atakuwa nchini Lesotho mwezi ujao tarehe 28, pamoja na  kumshukuru Mungu kutokana na kazi nzuri waliyoifanya na kundi zima la Spirit of Praise ambao walirekodi album yao ya 4 septemba mosi wiki iliyopita.

SIKU TANO ZA KUFUNGULIWA WAKAZI WA TANANGOZI NA VITONGOJI VYAKE

mhubiri friday kutoka mbeya akihubiri katika mkutano huo

baba onekana kwa watu wakoo sasaaaaaaaaaaa
Mtumishi wa mungu friday pamoja namwimbaji christopher mwahagila kutoka dar esalam

naja sanga mwimbaji kutoka mafinga akionesha utundu wake kwa yesu

mwimbaji jembe la yesu pamoja na elibariki shukia kutoka iringa

afisa mtendaji wa tanangozi nayepia wakati akiwasalimia wanaichi wa tanangozi


baadhi ya umati wa watu waliofika kwenye mkutano huo




kwa yesu raha eheeeeeeeee

washamba wanaomkataa yesuuuuuu


mtumishi wa mungu denis nyali pia naye alikuwepo

jembe la yessuuuuuuu

mchungaji mwenyeji wa kanisa la klpt staniley kiyeyeu pamoja na mwimbaji christopher

wakati wa baraka pokeaaaaaaaaaa

KWA TAARIFA YAKO--LIFAHAMU KANISA JIJINI DAR LENYE WAIMBAJI WENGI MAARUFU

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

KWA TAARIFA YAKO alhamisi ya leo ni kwamba kama tunavyojua kuna makanisa mengi nchini yamejaaliwa kuwa na waimbaji binafsi pamoja na vikundi vya kwaya ambavyo hutumika kumsifu Mungu katika ibada zao katika sharika hizo, ila pamoja na hayo kuna jambo hulijui ama walijua kuhusiana na kanisa la Evangelistic Assemblies of God (E.A.G.T) Mito ya baraka kwa askofu Bruno Mwakiborwa ambao wanapatikana mitaa ya kariakoo mkabala na klabu ya soka ya Yanga.

GK inaweza kuthubutu kusema kwamba kanisa hili ndio linaloongoza kwakuwa na idadi kubwa ya vikundi vya kwaya na waimbaji binafsi nchini ambao asilimia kubwa wote ni maarufu, kati ya waimbaji hao wanaopatikana katika kanisa hilo ni pamoja na Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Boniface Mwaitege, Ambele Chapanyota, J'sisters, Lugano Mwiganege, Rhema Singers, New Jerusalem Choir, Ebenezer Choir, Sifa John, Lyanga George, Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji na waimbaji wengine wengi ambao wanaendelea kumiminika katika kanisa hilo bila kumsahau kijana Silas Mbise ambaye ni mwalimu wa kwaya ya New Jerusalem pia mtangazaji wa Wapo Radio lakini kwwasasa nayeye ameamua kujikita kwenye muziki kama mwimbaji binafsi kwa kutanguliza single yake iitwayo Naja Bwana.

Kanisa hilo limekuwa na utaratibu wa kufanya uinjilisti sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam kwenye mikusanyiko ya watu kama Kariakoo, Karume na sehemu nyinginezo ambapo wamekuwa wakivuta umati wa watu na wengine kumpa Yesu maisha yao kutokana na injili wanayoisikia kupitia neno la Mungu pamoja na uimbaji unaobariki wengi.

J'sisters                         
Askofu Mwakiborwa akimtambulisha Masanja katika moja ya mikutano yao ya nje ya uinjilisti.                    
Flora na mumewe Emmanuel Mbasha katika picha ya pamoja.                        
Boniface Mwaitege na Bahati Bukuku wakifurahia jambo.
Baadhi ya vijana watanashati wanaopatikana kanisa la mito ya baraka.
Baadhi ya waimbaji wa New Jerusalem Choir watoto wa mito ya baraka katika picha ya pamoja.
Umati ukisikiliza injili maeneo ya Karume wakati kanisa hilo lilipokuwa likifanya uinjilisti eneo hilo.
Moja ya magari ya kanisa hilo yakiwa katika uinjilist

MAMA MZAZI WA MAREHEMU FANUEL SEDEKIA AFARIKI DUNIA

Marehemu Fanuel Sedekia.
Ikiwa takribani miaka minne tangu kufariki kwa mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa injili nchini Fanuel Sedekia huko nchini Israeli alikokwenda na msafara wa mwalimu Christopher Mwakasege kwa ajili ya kutembelea maeneo matakatifu naye mama yake mzazi Eunice Sedekia amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mount Meru jijini Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba mama huyo amefariki dunia usiku wa saa tatu hospitalini hapo, ambapo msiba na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Fanuel Sedekia maeneo ya White Rose jijini Arusha.
DAUD MWANGOSI SIKU MOJA KABLA YA KIFO CHAKE
katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard (Kulia) akifungua mkutano mkuu wa IPC jana katika ukumbi wa Maktaba ya Iringa katikati ni Daud Mwangosi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa IPC akifikiri jambo
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi (kushoto) akihojiwa na mzee wa matukio daima ambaye ni katibu msaidizi wa IPC juu ya wanahabari kudumisha umoja na mshikamano
Picha na habari zaidi utaendelea kuzipata hapa


Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari

JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog