Home » » Kasi ya Rais MAGUFULI imegonga hodi ofisi ya Rais-utumishi…hii ndio mikakati yao mipya!!

Kasi ya Rais MAGUFULI imegonga hodi ofisi ya Rais-utumishi…hii ndio mikakati yao mipya!!

Rais wa awamu ya tano Dk.John Magufuli ameendelea na mikakati yake ya kuhakikisha anaiweka nchi katika nafasi nzuri ya kufikia mafanikio ya kimaendeleo.
Ikiwa ni mwezi mmoja tangu achaguliwe kuiongoza nchi katika awamu ya tano, Rais Magufuli ameendelea kukaa kwenye headlines kufuatia maamuzi yake ya kuwaondoa watu wanaotumia vibaya madaraka yao ambayo yanaipeleka nchi katika wimbi la umaskini.
Kaimu katibu mkuu ofisi ya Rais Hab Mkwizu leo amekutana na waandishi wa habari, Dar es saalam na kuzungumzia utekelezaji wa utaratibu wa ahadi ya uadilifu kwa watumishi wote wa umma.
Katika mikakati waliyojiwekea Mkwiu amewakumbusha watumishi wa umma majukumu yao..“Kila mwajiri wa utumishi wa umma anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya Utaalam, uadilifu pamoja na uaminifu, pia anapaswa kuzingatia uzalendo na kuwahudumia wananchi kwa staa, kutoa huduma bora, usawa, kuheshimu sheria na kutumia vizuri rasilimali za Serikali kwa manufaa ya umma”...Hab Mkwizu.
Mwajiri atatekelezaje taratibu za ahadi ya uhadilifu?..”Kila mwajiri katika utumishi wa umma anapaswa kusoma na kuzingatia maelekezo yaliyomo katika waraka wa mkuu wa Utumishi kuhusu ahadi za uadilifu, pia atasaini kiapo kinachohusu watumishi wa umma kwa utaratibu uliowekwa na taasis husika”..
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog