Klabu ya soka ya Chelsea ambayo inashuka dimbani December 14 kucheza mchezo wake wa 16 wa Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/2016 dhidi ya klabu ya Leicester City. Chelsea
inaenda kucheza mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi 8
msimu huu katika mechi zake 15 za Ligi ambazo tayari imecheza.
Mara kadhaa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho
amekiri kuwa, moja kati ya vitu vinavyochangia kikosi chake kufanya
vibaya ni wachezaji kucheza chini ya kiwango, baada ya kuongea maneno
hayo mara kadhaa, December 13 Jose Mourinho amewataja wachezaji wake wanne ambao anafikiri hawako katika kiwango chao kama msimu uliyopita.
“Kama utaangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja utaona kuwa Branislav Ivanovic, Gary Cahill, John Terry msimu
uliyopita walikuwa na uwezo mzuri sana, lakini huu msimu ni ngumu
kusema mchezaji fulani yuko vizuri, uwezo wao karibu wote ni sawa, sioni
utofauti wa Cesc Fabregas na wala sioni akiogopa kukaa na mpira wala kufanya makosa” >>> Jose Mourinho
Klabu ya Chelsea wiki iliyopita ilipoteza mchezo wake wa nane wa Ligi Kuu Uingereza katika dimba lake la nyumbani Stamford Bridge dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu Bournemouth, licha ya kutwaa Ubingwa msimu uliyopita, Chelsea pamoja na kocha wao Jose Mourinho wapo katika wakati mgumu msimu huu.
0 comments:
Post a Comment