Headlines za kocha wa Man United Louis van Gaal
kuwa huenda taondoka klabu hapo zimekuwa zikichukua nafasi kila siku,
kwani mashabiki wa timu hiyo hawana imani na uwezo wa kocha huyo tena,
baadhi ya wachezaji wanahusishwa kuwa hawauelewi mfumo wa kocha huyo
ukilinganisha na wakati ambao yupo Sir Alex Ferguson.
Stori za Van Gaal kuhusishwa kufukuzwa kazi zimekuwa zikiandikwa ila December 5 kabla ya mchezo kati ya Man United dhidi ya West Ham United Louis van Gaal katoa majibu ya kuhusu hatma yake ndani ya Man United. Van Gaal yupo radhi kuondoka Man United endapo tu wachezaji wataamua aondoke.
“Mimi
ndiye kocha wa kwanza ambaye huwa naachia ngazi na hilo linathibitisha
kupitia klabu nilizofundisha pia kazi nilizozifanya, sidhani kama kuna
kocha yeyote ambaye huwa anaondoka mwenyewe tu au sababu ya pesa, ila
mimi nipo hivyo”>>> Van Gaal.
0 comments:
Post a Comment