Baada ya agizo la mashine za CT Scan na MRI kufanyiwa kazi, aliagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa kununuliwa vitanda baada ya kuona wagonjwa wengi wanalala chini.
Ikiwa ni sehemu ya juhudi zake leo Serikali ya Swizerland imesaini mkataba wa kuisaidia Tanzania kiasi cha bilioni 89.4 ambazo zitatumika katika huduma za afya katika kazi za msingi.
Wakisaini makubaliano Katibu mkuu wa Wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile pamoja na uongozi wa Serikali ya Swizerland tayari wamesaini mkataba huo ikiwa lengo kubwa ni kuimarisha mifumo ya afya.
“Serikali ya Swizerland wamekuwa nasi kwa muda mrefu, tutatumia fedha hizo vizuri na tutahakikisha hazipotei, msaada huu utakuwa na manufaa kwa wananchi wote”..italenga kusaida kupunguza vifo vya mama na mtoto, pia udhibiti wa ugonjwa wa Malaria”...Likwelile.
0 comments:
Post a Comment