JUMUIYA
ya Vijana wa Chama cha Wananchi (CUF) imesema wanasikitishwa na uteuzi
wa baraza la mawaziri lililotajwa juzi na Rais John Magufuli na kudai
kuwa, katika baraza hilo wamerudishwa wale mawaziri waliokumbwa na
kashfa za ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
Pia
imesema katika baraza hilo hakuna uteuzi ambao umewiana hasa katika
suala la usawa wa kijinsia na wala haukuzingataia Muungano uliokuwepo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuia
hiyo Hamidu Bobali amesema wanashangaa kuwaona aliyekuwa Waziri wa
Nishati na Madini Sospeter Muhongo na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi
Harson Mwakyembe kuwepo tena.
Amesema,
Waziri Muhongo alikuwa anatuhumiwa na suala la Escrow na akajiuzulu
halafu Magufuli amemrudisha tena kitu ambacho kinawakosesha amani.
“Inatusikitisha
sana kitendo cha Rais wetu kumteua tena Waziri Muhongo kurudi tena
wizarani hapo wakati alikuwa na kashfa kubwa ya escrow lakini
amerudishwa tena inaonyesha Magufuli pia pamoja na kusifiwa juu ya
utendaji wake hayuko makini,”amesema Bobali.
“Pamoja
na Muhongo pia Waziri Mwakyembe alikuwa katika wizara ambayo sasa hivi
inakubwa na matatizo makubwa ya kupitisha makontena na wakati alikuwa
waziri katika wizara hiyo, hilo lilitosha kwa Magufuli kufanya
upembuzi wa Mawaziri. Hao wote hawakufaa tena kuridi kuwa mawaziri,”
amesema.
Ameongeza
kuwa, wanasikitishwa sana kwani ile kasi ambayo Magufuli alianza nayo
wanaiona inakufa siku si nyingi kwa kuwarudia tena mawaziri hao mizigo.
“Wananchi
tunasikitika sana kwa kuwa tulimuamini Rais Magufuli lakini imani hiyo
inakaribia kukatika kutokana na kurudishwa kwa mawaziri hawa na
kusababisha kasi kupungua,”ameeleza
Aidha
aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo hakuwahi
kupatikana na hiyo ya Escrow kwani alijiuzulu mwenyewe. Kwa kuhofia
kupatikana na hatia.
Kwa
upande mwingine Mwenyekiti huyo alizungumzia mgogoro uliokuwepo
Zanzibar na kusema kuwa Baraza la vijana wa chama hicho kwa kushirikiana
na vyama vinavyunda Umoja wa Katiba Wananchi (Ukawa) wameandaa mkutano
juu ya kuzungumzia mgogoro huo.
“Tunafurahishwa
na mazungumzo yanayoendelea kati ya viongozi kwetu wa huko Zanzibar
lakini baraza letu limeandaa mkutano huo ili kuzungumzia suala
hili,”amesema Bobali
Hata
hivyo Bobali amesema wanamuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala la
Zanzibar kwani kutokufikia kikomo kunasababisha mambo mengi kurudi
nyuma ikiwa moja na uchumi kushuka.
“Jumuiya
ya vijana inawatahadharisha wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
kuacha mara moja kauli chafi na vitendo vya kichochezi vinavyofanywa na
wanachama hao kwani vinaweza kuamsha hasira za vijana wa CUF Zanzibar,”
amesema Bobali.
0 comments:
Post a Comment